Kampuni zote kubwa za Mitandao ya kijamii na Smartphone zina ofisi za uboreshaji wa teknolojia nchini Israel, wanalipwa kugundua ideas au feautures za kunogesha mitandao ya kijamii na simu.
Hata hivyo nchini Israel, kumekuwa na ongezeko au trend kwa watu kununua simu za zinazoitwa Kosher phones
Ni simu za mkononi zilizoundwa au kurekebishwa ili kuzuia intaneti, mitandao ya kijamii, Ai na maduka ya programu (app stores), huku zikiruhusu huduma za msingi za mawasiliano.
wanaotaka kuongea kwenye magroup wanakutana kijiweni au kupanga kikao kama zamani, wanaotaka taarifa wanasikiliza radio, wanaotaka kucheza magemu wanakutana sehem kucheza kama zamani, wanaotaka Chat Gpt wanaenda maktaba wasome vitabu au kutumia akili zao kama zamani