Nyie mnaomshikia bango,
Wenyewe mnasema kinamatatizo fulani kimeficha kwenye kifua. Frustration hizo zinampeleka mtu kusema mambo mengi ambayo huwa hayatakiwi kusemwa. Nimeshaona watu kama hao wengi sana. Waarabu, Waethiopia, Mamulato nk ambao wakiwa na Wazungu, hujifanya kuwa wao si Waafrika. Nilishawahi kukaa na kijana kutoka Guyana English (kwa akina Edy Grant). Huyu jamaa mwanzo alikuwa akijiita yeye ni Mu-America. Akawa anashangaa sisi tuna pesa kumzidi hata yeye.
Hao wengine juu walikuwa wakienda kwa Wazungu wakipigwa Kibuti, ndiyo wanarudi na kujifanya eti na wao Waafrika. Sisi tulikuwa tunawacheka tu na wala hilo halitupi kabisa pressure. Cha ajabu wakifika kwenye Disco, utashangaa na wao wanataka BIG, 2Pac, Blackstreet, Kut Close, Whitney Houston, Bobby Brown, Jay-z nk
Huyo dada na nyie wote mnaomshupalia, wote mko sawa. Kama kasema au hakusema, hajawahi kumegwa au kamegwa na Mpingo, wewe linakuhusu nini? Na hata kama alikuwa akitembea na Mpingo na wakalala kitanda kimoja, una uhakika gani kwamba jamaa alimega? Wanaume wangapi hujisifu kuwa amemega kumbe ukweli ni kuwa kijogoo hakikusimama au mdada yuko kwenye siku zake?
Burn homeboy, drop kabisa hilo wazo la kwenda kumhoji maswala hayo. Labda kaa naye na ufanye utafiti ni kitu gani kimemsibu mwenzetu na kumpa tu ushauri awaombe hata watu wake wa karibu au Wazee wa busara na wao watampa mawazo mazuri tu. Umkanye mambo ya kuropoka ropoka na akiweza kama mmoja alivyoshauri, basi aende shule. Shule itamsaidia kuanza kupima yale anayoyasema na asiwe mtu wa kuropoka vishekesho.
Burn, kama huyo dada anasema "angelipata laki mbili basi angelikuwa among 5 richest Tanzanias" basi huyu ndiyo wa kuumbuwa? Si wa kuonea HURUMA na kumsaidia? Inabidi wampeleke Kahama, akaone matajiri wa pale wengi tu wanazidi hizo pesa.
Nendeni mumpe ushauri, auze magari yake na aende shule. Vitu anavyosema hadi vinatisha. Shule itampa fursa ya kuiangalia hii dunia vingine kabisa. Tafadhali, tafadhali, Watanzania tubadilike. Tusiwe watu wa kuangalia na kucheka mtu. Tuangalie kwa nini hali iko vile na kumsaidia mtu. Wakati Brenda Fassie kawa mbugia miunga, hadi siku moja wameokotwa akiwa HOI na rafiki yake ameshakauka, hawakumpiga picha na kumuacha ajifie mwenyewe. Walielewa kuwa binti sifa zimemzidi na kasindwa kuvumilia. Alilazwa na kutibiwa chini ya usimamizi wa Madiba na mwenyewe na alipopona, hata nyumbani kwake hakurudi. Yeye alienda kukaa kwa rafiki yake wa Jela Mandela aitwaye Tokyo Sexwale. Mtoto wake alipelekwa kwenye familia ya Mbeki na baadaye UK. Hivi ndivyo inatakiwa kuwa. Mipingo tunatia aibu maana hata Tembo wanatuzidi. TUBADILIKE SISI WOTE (hata mie).