DOKEZO Wazabuni Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wapaziwe sauti

DOKEZO Wazabuni Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wapaziwe sauti

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Undule Lumuli

Member
Joined
Mar 24, 2025
Posts
6
Reaction score
5
Hapa Halmshauri kwetu (Rungwe ) Mkoa wa Mbeya kuna baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wamekuwa wakitoa huduma ya Zabuni ya kulisha Shule za Sekondari za Serikali, Magereza na Chuo cha ufundi kwa muda mrefu, lakini kwa bahati mbaya PESA ZAO hawalipwi kwa wakati ama hawalipwi kabisa

Wamekuwa wakija hapa Ofisini kufuatilia mara kwa mara lakini hawaambilii chochote, Imagine kuna baadhi yao wanadai pesa toka mwaka 2009 kuna baadhi wamekufa, wengine wameacha hiyo kazi, na hata waliobaki sidhani kama wanaweza kuendelea kwa muda mrefu.

Jambo hili limefanya wananchi hawa kuingia kwenye madeni, kutishiwa kufungwa kwasababu walichukua chakula kwa watu kwa mali kauli lakini Serikali haiwalipi.JF wapazieni sauti hawa wazee maana wakija hapa ofisini unaona kabisa hawako sawa ila hatuna namna ya kuwasaidia...WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO fuatilieni madai haya, Spika wa Bunge huku kwenu Halmashauri inataka kukuchafulia jina na hawa ndo wapiga kura wenu.

WAZABUNI WALIPWE, WALIPWE, WALIPWE hizo ndo ajira zao ambazo Familia zao wanawategemea, walipeni ili wakae kwa amani na walipe madeni wanayodaiwa... MKURUGENZI walipeni hawa wazee mnabeba laana mjue
 
Back
Top Bottom