Wazalendo saba waliolala usingizi wa R.I.P Van Winkle

Wazalendo saba waliolala usingizi wa R.I.P Van Winkle

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WAZALENDO SABA WALIOLALA KIMYA KWA MUDA MREFU NDANI YA SEFU YA ALLY SYKES
Hukaa kimya fikra zangu ghafla zikagutushwa na kitu nikakigeuza ndani ya kichwa changu kisha nikajiuliza ilikuwaje, nani alihusika na nini sababu yake?

‘’Nakumbuka kama jana Ally Sykes ananyoosha kidole ukutani ofisini kwake Mtaa wa Makunganya kuniambia, ‘’Nina file nyingi ndani ya sefu hapo.’’

Naangalia lakini siioni hiyo sefu ninachoona ni ukuta na kabati kubwa.

Nimeingia ofisi hiyo mara nyingi lakini hakunipitikia kuwa pale kuna sefu.

‘’Sijua ufunguo wake uko wapi lakini nitautafuta ikiwa sitaupata nitamwita fundi aje tuvunje.’’

Jumatano ilipofika nimekwenda ofisini kwa Ally Sykes.

‘’Nimeziona funguo za sefu.’’

Ally Sykes akasimama kutoka kwenye meza yake akaenda ukutani akavuta milango ya kusukuma (sliding) ya kabati akafungua sefu na kuanza kutoka mafaili.

‘’Chukua mafaili hayo yasome ukimaliza njoo tuzungumze.’’
Imekuwaje tumefika pale Ally Sykes kuitolea mafaili yake?

Joseph Kasella Bantu alikuwa ameandika makala katika gazeti ya New African akieleza masikitiko yake kwa historia ya TANU kutopewa umuhimu unaostahili.

Mimi nilimuunga mkono Kasella Bantu katika toleo lililofuata lakini nikasema kama nikutoa msaada Kasella Bantu atakuwa katoa msaada gani wa kumshinda Abdul Sykes?

Ally Sykes alipedezewa sana na majibu yangu akamtuma mwanae aniite nikamuone.

Ndipo nikamwambia kumaliza haya matatizo ya historia ya TANU bora niandike kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Ally Sykes akaniambia kuwa amekuwa na fikra ya kutafuta watafiti kuandika historia ya marehemu kaka yake lakini hajalifanya hilo.

Nikamuomba mimi hiyo kazi.
‘’Mohamed wewe kweli unaweza kuandika?

Hivi ndivyo ikatokea kwa Ally Sykes kunikabidhi nyaraka zile.

Kuanzia file la kwanza nilipoanza kusoma nilikuwa natoka katika miaka ya 1980 najikuta niko katika Tanganyika inayotawaliwa na Waingereza.

Nilikuwa kama mtu niliyepagawa.
Akili yangu haifikiri kitu chochote isipokuwa utafiiti uliokuwa umenikabili.

Nilimwambia Ally Sykes baada ya kupitia nyaraka chache kuwa siwezi kusubiri hadi nimalize kusoma mafaili yote.

Ally Sykes akanipangia kila Jumamosi nakwenda ofisini kwake namhoji nay eye anazungumza na mimi namrekodi kwenye cassette player.

Katika mazungumzo yetu alitoa amri kwa katibu muhtasi wake Bi. Zainab kuwa hataki simu wala hapokeI mgeni.

Ni kama vile hivi sasa Ally Sykes yuko mbele yangu anazungumza na mimi ofisi yote kimya ila kwa sauti ya kinasa sauti kikizunguka na kutoa sauti ya chini.

Leo nataka nikuwekeeni hapa picha za wazalendo saba waliolala usingizi kwa miaka mingi ndani ya sefu ya Ally Sykes hadi siku nilipowaamsha na wakaamka kutoka Dar es Salaam ile ya miaka 1920 wakajikuta wako katika Dar es Salaam nyingine kabisa ya 1980.

Watu hawa walikuwa wamelala usingizi fofofo wa zaidi ya nusu karne.
Hii kwangu ilikuwa hadithi ya Rip Van Winkle.

Kila aliyewasoma lau kama walikuwa wanawajua kwa kuwaona na wengine kwa kuwasikia walikuwa wakishangaa na kujiuliza watu hawa walikuwa wapi miaka yote hii?

Haya tunayosoma ya kweli au porojo?

Ukwei ni kuwa hawa wazalendo walikuwa ndani ya sefu ya Ally Sykes kwa miaka wakisubiri kuamshwa.

Walipotoka usingizini na kuamka niliwaomba wanipe no. za kadi zao za TANU walizokata mwaka wa 1954 baada ya TANU kuasisiwa:

1. Julius Kambarage Nyerere Kadi No. 1
2. Ally Kleist Sykes Kadi No. 2
3. Abdulwahid Kleist Sykes Kadi No. 3
4. Dossa Aziz Kadi No. 4
5. Denis Phombeah Kadi No. 5
6. Dome Okochi Budohi Kadi No 6
7. Abbas Kleist Sykes Kadi No. 7
(Kuna taarifa nyingine zinasema kuwa kadi No. 7 ni ya John Rupia)

Picha zote ingia hapo chini:





243977994_1037081987039179_2255883923773096833_n.jpg
 
Hawa wakina sykes mzee unaonekana kuwahusudu sana.
Waterloo,
Hii ni historia ambayo ni sehemu ya maisha yangu.

Nazaliwa hawa wazee wananiona mtaani nami nawaona na najua historia ya uhuru ilivyokuwa.

Niko kijana nafundishwa historia Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam historia ninayofunzwa si historia ninayoijua.

Hujashangazwa na majina haya mawili la Denis Phombeah na Dome Okochi Budohi katika majina saba ya wanachama wa mwanzo wa TANU?

Mbona hawa wamebadilisha historia ya TANU?

Nia yangu nakutakeni muijue historia hii kwa ukamilifu na pasiwe na shaka yoyote kuwa historia iliyoko si historia ya kweli.

Nawahusudu sana wazee wangu hawa.

Kama nisingeandika historia hii ningejidhulumu mimi mwenyewe na kuwadhulumu wazee wangu.
 
Katika nyakati za zama zao,si tu walikuwa wazalendo bali pia walikuwa wajasiri. Kuanzisha chama Cha Siasa kwa lengo la kudai uhuru toka kwa utawala wa kikoloni!
 
Mambo ya hizo kadi na maisha ya sasa ni mbingu na nchi
Google...
Hakika kilichobaki ni raha ya kuwasoma wazalendo waliosahauliwa na wanahistoria wetu.

Ungemjuaje Dome Budohi ,"The Mau Mau," ndani ya TAA na TANU?

Kanihadithia kwa mdomo wake alivyokamatwa na Special Branch 1955 na kupelekwa Handeni kwenye kambi ya Mau Mau akisubiri kupelekwa kifungoni Lamu.

Ungependa nikuhadithie kisa chake chote nikuwekee na picha nilizopiganae 1972 nikiwa na umri wa miaka 20?

Dome akinijua mimi na wazee wangu wakati ule wa kupigania uhuru.
 
WAZALENDO SABA WALIOLALA KIMYA KWA MUDA MREFU NDANI YA SEFU YA ALLY SYKES
Hukaa kimya fikra zangu ghafla zikagutushwa na kitu nikakigeuza ndani ya kichwa changu kisha nikajiuliza ilikuwaje, nani alihusika na nini sababu yake?...
Heshima yako Mkuu!?

Hivi Kuna uhusiano Kati ya Dossa Aziz na Rostam Aziz?
 
Google,
Nimezaliwa 1952.

Huu ndiyo mwaka Mwalimu Nyerere anafika kwa Abdul Sykes.

Abdul Sykes ndiye aliyemjulisha baba yangu Nyerere.
Pokea shikamoo yangu mkuu ww ni babu yangu maana hata baba angu hakuwa amezaliwa mwaka huo
 
Hapo ndipo lilipo tatizo na home boy wangu! Kwake yeye historia ya Tanzania/Tanganyika ni ukoo wa Sykes
Kichuguu,
Haiwezekani historia ya nchi nzima ikawa katika ukoo mmoja.

Sijui kwa nini umeita tatizo.

Ikiwa na wewe unalo la kuandika kuhusu wazalendo waliokuwa kwenu ulikozaliwa ieleze tutaisoma.

Historia hii umuhimu wake unakuja kwanza ni kuwa ilifutwa na ikawa haipo.

Matokeo yake watu wakaamini historia ambayo siyo.

Hata nilipoandika historia hii ambayo ndiyo historia ya kweli wapo mfano wa wewe inawaudhi.

Hii mosi.

Pili historia hii mimi ni sehemu ya maisha yangu na baadhi ya wengine wa kizazi changu tuliozaliwa miaka hiyo.

Ikiwa hii historia huipendi kuona inahadithiwa acha kusoma utakuwa umesalimika.

Ikiwa unanisoma hapa JF utaona kuwa nimekuwa nikifanya mahojiano na vituo kadhaa za televisheni binafsi na TBC.

Huu ni mwamko mpya ambao umenitia moyo sana.

Lakini kubwa ni shinikizo kutoka kwa jamaa zangu kuwa niandike maisha yangu.

Haya unayosoma hivi sasa ni kwa ajili ya hawa wanaotaka kunijua zaidi na kujua hali ya siasa ilivyokuwa Dar es Salaam wakati wangu.

Nataka badala ya kusoma maisha yangu ambayo hayana kitu wawasome hawa wazee wangu.

Ndugu yangu usijiudhi bure.
Acha tu kusoma.

Historia ya Mwalimu Nyerere na TANU na harakati za kudai uhuru wa Tangayika ni sehemu ya historia ya ukoo wa Sykes na sehemu ya historia ya babu yangu Salum Abdallah.

Salum Abdallah ni muasisi wa TANU Tabora na pia muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) mwaka wa 1955.

Juhudi za kuwafuta hawa wazee wangu ndiyo haya sasa unanisoma mimi.

Screenshot_20211005-085806_Facebook.jpg


Screenshot_20211005-075828_Facebook.jpg
 
Kichuguu,
Haiwezekani historia ya nchi nzima ikawa katika ukoo mmoja.

Sijui kwa nini umeita tatizo.

Ikiwa na wewe unalo la kuandika kuhusu wazalendo waliokuwa kwenu ulikozaliwa ieleze tutaisoma.

Historia hii umuhimu wake unakuja kwanza ni kuwa ilifutwa na ikawa haipo.

Matokeo yake watu wakaamini historia ambayo siyo.

Hata nilipoandika historia hii ambayo ndiyo historia ya kweli wapo mfano wa wewe inawaudhi.

Hii mosi.

Pili historia hii mimi ni sehemu ya maisha yangu na baadhi ya wengine wa kizazi changu tuliozaliwa miaka hiyo.

Ikiwa hii historia huipendi kuona inahadithiwa acha kusoma utakuwa umesalimika.

Ikiwa unanimous hapa JF utaona kuwa nimekuwa nikifanya mahojiano na vituo kadhaa za televisheni binafsi na TBC.

Huu ni mwamko mpya ambao umenitia moyo sana.

Lakini kubwa ni shinikizo kuwa niandike maisha yangu.

Haya unayosoma hivi sasa ni kwa ajili ya hawa wanaotaka kunijua zaidi na kujua hali ya siasa ilivyokuwa Dar es Salaam wakati wangu.

Ndugu yangu usijiudhi bure.
Acha tu kusoma.

Historia ya Mwalimu Nyerere na TANU na harakati za kudai uhuru wa Tangayika ni sehemu ya historia ya ukoo wa Sykes.

Juhudi za kuwafuta ndiyo haya sasa unanisoma mimi.
Home boy, kuna vitu huwa unaifurahisha kwa kuleta facts ambazo zilikuwa hazijulikani, lakini pia kuna facts ambazo huwa unazipa mkazo wa kupitiliza kiasi, na hapo ndipo tatizo linapokuja.
 
Back
Top Bottom