Wazalishaji wa pombe aina ya banana mkoani Arusha wanailalamikia TRA

nguluvisonzo

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
515
Reaction score
71
Baada ya selikali kupitia waziri mkuu akiagiza wazalishaji wote wa pombe wafunge mashine zitakazo kuwa zina bandika stempu za kodi mpaka sasa ni banana investment tu ndie aliye aandikishwa TRA Arusha wengine bado na wanalalamika kuwa wamekamilisha kila kitu,kuna nini hapo,Meneja wa TRA Arusha kulikoni?selikali ilitoa maagizo hayo ili iweze kukusanya kodi pasipo kupoteza mapato nyinyi mnachelewesha zoezi,wengine wanamikopo toka wasimame inakuwaje?au mpaka JPM aseme ndio mtekeleze?waziri wa Fedha mulika hawa watu wanakuangusha,waliopo Arusha toeni taarifa mbona mna mkuu wa Mkoa mchapa kazi,mtumieni.Takukuru Arusha fuatilieni hao TRA Arusha kuna jambo hapo.
 
Huko A town vip kwanini msiende kwa mh waziri?mkuu wa mkoa wenu anasemaje? mpigieni simu kamishna mkuu wa TRA ikishindikana mnajiunganisha mnaandika barua ya pamoja na ya wazi kwenye magazeti kwenda kwa mh. Magu.......TBC 1 ipo kwa ajili yenu itumieni pia wabunge watumieni ipasavyo. Tafuteni mawasiliano ya ikulu mpeleke kilio chenu
 
Mkuu Hao wengine wanaolalamika wamekamilisha kila kitu wamekupa uthibitisho wa kukamilisha nyaraka zote? kama siyo taarifa umeitoa wapi? kama ndio Kwanini wamekupa wewe huo uthibitisho? Una tengeneza aina hii ya kinywaji na umekamilisha taratibu zote ila hujapata hitaji lako? Umeandika kama mtu mwenye information sana kuhusu hili soko kiasi cha kuletewa malalamiko na wahusika au ni wewe unafanya hii biashara na umekwama sehemu. Funguka vizuri usaidike usije sababisha watu wakaondolewa makazini kwa mambo ambayo kumbe yangeweza kutatulika au yamekwama sehemu za chini huko au wahitaji huduma ndo wenye shida.
Nikukumbushe tu Mwanasiasa anachoangalia siku zote ni wengi wape, Hashindwi kumtoa mtu kafara ili mambo yaende, sasa kama kitu kinaweza kutatulika bila kufikia uongozi wa kisiasa basi kitatuliwe.
kabla hatujaleta uchochezi wa kuharibiana kazi tuhakikishe kweli inastahili kufikishwa mbele. Kwann hujawashauri waungane wamwandikie barua commissioner wa TRA wasikie majibu kama wasiporidhika ndo waende mbele? Una hamu ya kusikia mtu katumbuliwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…