Wazaliwa wengi hawamiliki mijengo Dar

Wazaliwa wengi hawamiliki mijengo Dar

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Hii tafiti nimeiona kwa wengi. Wazaliwa wengi hasa wale waliokuta nyumba za familia hawamiliki mijengo. Wengine waliojisogeza wanamiliki kiwanja lakini kujenga anasubiri kikokotoo.

Wale wa kuja wengi baada ya miaka mitano au chini ya hapo, anamiliki mjengo. Wengi waliniambia ni hasira ya kulipa kodi, masimango ya wenye nyumba ndivyo vimewasukuma.

Hawa wazawa wengine wanafurahisha. Mtu anaanza familia kabisa akiwa kwenye guest wing ya shemeji. Siku shemeji amempiga dada inabidi uwe upande wa shemeji usifukuzwe kwenye nyumba. Unamwambia dada avumilie ilhali damu imevilia kwenye jicho.
 
Wengi watapita kimya kimya hapa ukweli mchungu.
 
Nijenge nini mzee kaacha nyumba za kutosha. Kujenga bila kuwa na mradi endelevu ni uoga wa maisha.
 
Na watoto wa kaka zako na wa dada zako hizo mali zitagombaniwa kama league juu ya England
Kwa wasio na elimu watafanya hivyo! ! Ila siwezi Kujenga harakaharaka kama wafanyavyo wakuja tena kwa mikopo kila mahali.
 
Hii tafiti nimeiona kwa wengi. Wazaliwa wengi hasa wale waliokuta nyumba za familia hawamiliki mijengo. Wengine waliojisogeza wanamiliki kiwanja lakini kujenga anasubiri kikokotoo.

Wale wa kuja wengi baada ya miaka mitano au chini ya hapo, anamiliki mjengo. Wengi waliniambia ni hasira ya kulipa kodi, masimango ya wenye nyumba ndivyo vimewasukuma.

Hawa wazawa wengine wanafurahisha. Mtu anaanza familia kabisa akiwa kwenye guest wing ya shemeji. Siku shemeji amempiga dada inabidi uwe upande wa shemeji usifukuzwe kwenye nyumba. Unamwambia dada avumilie ilhali damu imevilia kwenye jicho.
Utafiti fake dada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kabisa wala siyo utani...

Haswa kama umekuta wazazi tayari wameshawajengea mijengo na kusema hii itakua ya kwako na hii itakua ya fulani... zile nyingine ziachane zitawasidie mbeleni...

Inatia uvivu sana kujenga ya kwako...

Cc: mahondaw
 
Ukizingatia viwanja vipya Mambwepande hukoo.

Leo ninawaongelea wale waliojistiri kwenye guest wing ya shemeji.
 
Mambwepande mbona mbali hukoo...
Vipo hapo tu Bunju, vinaanzia laki nane...

Hao waliyojisitiri kwa mashemeji lazima kupambana wajenge...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom