Wazamani (wahenga) tukutane hapa

maiyanga1

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
1,340
Reaction score
1,832
Naamini kila mmoja wetu anachukua tahadhari kujikinga na COVID 19.

Je, mhenga mwenzangu unakumbuka dMt, Co cabs, MORETCO, TADECO, CORETCO?

Je, unakumbuka magazeti gani ya zamani, ambayo ukiwa nje ya mikoani gazeti la leo unalisoma baada ya siku mbili?

Je unakumbuka majumba ya sinema na picha zake zilizohit?

Je unakumbuka kumbi gani za starehe zilizokuwa zinawaka moto weekend?

Je unakumbuka Taarifa ya Habari ya saa mbili usiku ilivokuwa muhimu kwa watu aidha kutumbuliwa au kuteuliwa?

Je unakumbuka jinsi vijana walivyokuwa mashujaa wanavyozamia meli kwenda nje?

Wadada wa zamani mnakumbuka mlivyokuwa mnachoma nywele ili kukonga nyoyo za wanaume?

Hebu tukumbushane, ya kale ni dhahabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe,DDC (Kariakoo/Magomeni Kondoa),Imasco,Lang'ata,Mambo club,Rungwe oceanic,Silver sands,Msasani beach,La Dolce vita,Casanova
Uhuru,Mzalendo,Mfanyakazi,Daily News,Sunday News
Empress,Empire,Avalon,New chox,Cameo,Odeon,Drive-in cinema
Kuna meli moja ya kubeba magari ilikuwa inakuja(car carrier) ina mlango mkubwa nyuma unatumika kushusha magari ilikuwa inaitwa MV Kishtobe ndio chanzo cha mademu kuitwa Kishtobe
Wengine walikuwa wanapaka KANYA na YOMBOO ili nywele ziwe nyeusi
Marhaba mtoto mzuri
Hahahaha, mkongwee safi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…