kipindi tunakua mtaani hakukuwa hata na nyumba moja yenye fensi, yaani mtaani watoto wote tulikuwa tunajuana kama ndugu, mkirudi shule na wakati wa likizo wote mko pamoja ni kucheza kwa kwenda mbele.
nawahurumia watoto wangu, maana they will never experience that kind of socialization. full time wako ndani ya geti na mtaa wote ni mageti tu.
style ya maisha imebadilika sana.
nikiwa shule ya msingi nilikuwa natumwa hadi sokoni kariakoo au ilala. lakini kwa sasa mtoto wangu wa form II nasita kumtuma sehemu za namna hiyo na kwanza siamini kama anaweza manage hizo hussle.
all in all zamani ilikuwa ni tamu sana. labda tu tulimiss social media kama jf,