bashitegufu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2017
- 201
- 117
Unakumbuka wimbo wao uliimbwa binti mmoja unaimbwa 'watoto wasafi moyoni Ni nyota za macho ya wazazi,sisi ni maua tuliopendwa na Mungu mwenyenzi'Pia kulikuwa na ile band ya vijana wa Kihindi, VARDA ARTS.
Ilikuwepo pia Edition Mulanga studio kule Temeke.Kizenga Recording,Casino recording, zilikuwa manzese.kariakoo shahista na Elricard recording, nyingine ilikuwa Buguruni Jina nimesahau
Ilikuwa poa sana hiyo nyimbo. Sijui yupo wapi yule mwanadada?!Unakumbuka wimbo wao uliimbwa binti mmoja unaimbwa 'watoto wasafi moyoni Ni nyota za macho ya wazazi,sisi ni maua tuliopendwa na Mungu mwenyenzi'
Kama sikosei lilikuwa ni kundi la Varda arts ndio walioimba ule wimbo.Ilikuwa poa sana hiyo nyimbo. Sijui yupo wapi yule mwanadada.
Mkuu ukiwaambia vijana wa sasa kwamba pale ulipo ubalozi wa USA ndio kulikuwa na Drive-in cinema hawatakuelewa....enzi hizo kama huna hela unakaa pale nje unacheki Bruce lee na akina Fred Williamson bila sauti. Tulikuwa tunaita kiingilio mbu!
Jamhuri photo studio,, mtaa wa kaliua na morogoro road,, hii studio ni ya kitambo asee pande za mwembe chaiKuna muhenga alieifahamu GLC PHOTO STUDIO kinondoni mtaa wa ufipa pale?
Enzi zile late 70's
Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah huyu mzee kitambo sana, watoto tulikuwa tunamuogopa sanaKuna Mzee mwengine alikuwa anaitwa Mzee Majambo anauza karanga anavaa na manyanga mguuni...!
Daah mwamba umekulia katika hood kama yangu , gari la koni za Bakhressa.Kabisa kabisa kiongozi alikuwa na karanga tamu kabisa akipita yeye baadae likipita gari la koni unashushia aisee.
Acha kabisa mkuu...!