Wazamani (wahenga) tukutane hapa

Yeah ukiwa kikojozi akipita huyu mzee lazma wakupeleke kwake na alivyokuwa anatisha aisee lazma uache kujikojolea mkuu. 🤣🤣🤣
Ila alikuwa anauza karanga nzuri balaa! Tatizo ukimsikia na manyanga yake anakuja unakimbia unaenda kujificha chini ya kitanda!
 
Ila alikuwa anauza karanga nzuri balaa! Tatizo ukimsikia na manyanga yake anakuja unakimbia unaenda kujificha chini ya kitanda!

Kabisa kabisa kiongozi alikuwa na karanga tamu kabisa akipita yeye baadae likipita gari la koni unashushia aisee.

Acha kabisa mkuu...!
 
Kuna jamaa walijitokeza kwenye makaburi ya Kinondoni wakiwa wamevaa sanda na maudongo udongo kama vile wamefufuka hivi, sasa upande wa pili wa barabara kulikuwa na bar pale mwembe jini kukiwa kumepaki gari kama zote aisee, unakumbuka kilichotokea mkuu...? 🤣🤣🤣
 
Wale wezi walitumia akili kubwa sana! Kuna mtu na mkewe walikutana home asubuhi kila mtu alikimbilia upande wake. Magari waliyafuata mchana siku iliofuata.
 
Wale wezi walitumia akili kubwa sana! Kuna mtu na mkewe walikutana home asubuhi kila mtu alikimbilia upande wake. Magari waliyafuata mchana siku iliofuata.

Hahahahah hapo mwisho nimecheka sana aisee...! 🤣🤣🤣
 
Safari Resort Bar nyumbani kwa OSS wana Ndekule/ Masantula/ Dukuduku. White House Kimara, nyumbani kwa Orchestra Maquiz Du Zaire wana Kamanyola bila jasho/ Sendema.

Nawakumbuka Dar International Jazz (Super Bomboka), UDA Jazz (Bayankata), Urafiki Jazz (Wana chakachua), Orchestra Magoma Moto ( The Big mayai), Tancut Almas (Fimbo Lugoda), Lola Afrika, Kurugenzi Jazz ya Arusha, Mwenge Jazz, Orchestra Kyauri Voice.......

Dah, enzi za vipindi vya RTD Idhaa ya Biashara kama vile Misakato, Ombi lako cha Selemani Muhogola, Club Raha Leo cha uncle J, Mambo mpwito-mpwito cha Charles Hillary, African Rythim cha Stephen Lyimo pale RTD Externa Service. Vipindi vya Idhaa ya Taifa ya RTD kama vile Usalama Barabarani, Ukulima wa kisasa, Ujumbe wa leo, Mikingamo cha Ahmed Kipozi.....yaani long time......Ama kweli siku hazigandi.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naongezea.
Magereza jazz, Mzee Makassi, polisi jazz, kumbakisa, kimbunga jazz, uda nao walikua na bendi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Empress, Empire, Avalon, New chox, Cameo, Odeon, Drive-in cinema
Avalon niliikuta na walikuwa bado wanaonyesha Cinema. Ila Drive in ilikuwa ni uwanja tu walikuwa hawaonyeshi kitu.

Kwa vijana wa leo Avalon ilikuwa Posta ya zamani ubavuni mwa Kanisa la St Joseph, Drive in ndio wamejenga Ubalozi wa Marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…