MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Miaka kadhaa iliyopita kuna picha ili-trend sana mitandaoni ya Waziri mstaafu wa kilimo wa Zambia kuonekana amempigia magoti Rais mstaafu Edgar Lungu (nimeipost). Watu wengi sana walitoa maoni yao na wengine kufikia hatua ya kumlaani Rais Lungu kuwa ni dikteta anayedhalilisha watu wake. DC wa Tunduru, Mtatiro alikuwa miongoni mwa watu maarufu kupost na kuonyesha kukerwa na picha ile.
Binafsi pia nilikerwa mno na kumwona Rais Lungu kama mtu asiyefaa bila kujua kwa wazambia lile lilikuwa suala la kawaida sana. Yaani ni ishara tu ya kuonyesha nidhamu na wala hakuna baya. Ukimtembelea Mzambia basi utakutana na jambo litakalokushangaza sana. Mke wa mwenyeji wako (shemeji) akiwa anakupa maji ya kunywa lazima apige goti na atainuka ukishaweka glass ya maji chini baada ya kunywa. Pia wakati wa kukuitia msosi lazima apige goti ule muda anaposema "shemeji karibu"...
Mimi kwa kweli nataka huu utaratibu uletwe huku kwetu tuone kina Mdude Chadema akimpigia goti Mzee Kinana wanapokutana kwenye sehemu kama sherehe. Au Manara kumsalimia Karia kwa kupiga goti. Ni mambo ya nidhamu.
Nimekuwekea picha kadhaa ujionee hali halisi;
1. Waziri wa kilimo mstaafu akiwa kapiga goti mbele ya Rais mstaafu Lungu.
2. Rais Hakainde Hichilema aliyepiga magoti akimsalimia Chifu Chitimukulu wa kabila la Bemba.
3. Mbunge wa upinzani Chitalu Chilufya akisalimiana na Rais Hakainde Hichilema walipokutana kwenye sherehe za Umutomboko.
4. Rais mstaafu Edgar Lungu na mkewe Esther Lungu (wa kwanza kulia) wakisalimiana na makamu wa rais (aliyepiga goti) Mama Mutale Nalumango.
5. Wabunge wa chama cha upinzani PF walipomtembelea Chifu Mwata Kazembe.

Attachments
-
IMG_20220413_190039.jpg80.5 KB · Views: 14 -
IMG-20220508-WA0013.jpg34.6 KB · Views: 13 -
FB_IMG_1659361862723.jpg32.5 KB · Views: 12 -
IMG-20220508-WA0011.jpg48.3 KB · Views: 13 -
FB_IMG_1659188337438.jpg38.5 KB · Views: 13 -
IMG-20220508-WA0012.jpg30 KB · Views: 13 -
FB_IMG_1659188327722.jpg57.1 KB · Views: 13