Labda kama hukuwepo wakati ule, watu walikuwa wanatoa maoni kwa uhuru kabisa na wala hakukuwa na questionnaire ya kujaza!
Hakuna uhuru wa kutoa maoni kama kujadili kuvunja muungano ni kosa la uhaini.
Hilo kosa linatakiwa kuondolewa kwanza kabla ya wewe kuweza kusema kwamba watu walitoa maoni kwa uhuru.
Ukisikia Wazanzibari wanasema wanataka serikali tatu au wanataka serikali ya mkataba, hiyo ni uephemism.
Euphemism ni neno la Kiingereza, maana yake ni kutumia neno au dhana isiyo na makali sana, wakati unamaanisha jambo lenye makali zaidi.
Kwa mfano, mtu anaenda chooni, lakini hasemi anaenda chooni, anasema anaenda "uani".
Nafikiri kwa Kiswahili euphemism inaitwa tafsida.
Sasa Wazanzibari wengi wakisema wanataka muungano wa serikali tatu, muungano wa mkataba etc, hiyo mara nyingi ni euphemism, wanasema wanaenda uani wakati wanamaanisha wanaenda chooni.
Wengine wanataka kuuvunja muungano, ila wanaanza polepole kwanza.
Wapewe nafasi tu kupiga kura katika kura ya maoni ya huru na haki.
Kura hii itakuwa na faida mbiki.
Kama Wazanzibari wengi wanautaka muungano, tutalijua hilo na muungano utaimarika, wasioutaka watajulikana kuwa ni wachache.
Na ikiwa Wazanzibari wengi hawautaki muungano, kura hii itawapa nafasi ya kuondoka kwenye muungano na kuanzisha nchi yao wenyewe tuondokane na kelele za kila mara kuhusu muungano.