Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
WAZANZIBARI NA IMANI YAO KWA ALLAH
Rais Hussein Mwinyi kafungua msikiti uliopewa jina lake.
Jina la msikiti huo litabaki siku zote kuwa Masjid Hussein jina la mjukuu wa Mtume SAW.
Rais Mwinyi akaombewa dua na Waislam na yeye akashukuru kwa hilo.
Hawa ndiyo Wazanzibari walioutanguliza mbele Uislam wao na kuupokea mwito wa Allah kuwa Waislam ni ndugu.
Naamini bila ya chembe ya shaka kuwa Rais Hussein Mwinyi anajua uzito wa dua hizi anazoombewa na yeye akiwa kasimama kibla kanyanyua mikono anaitika Amin pamoja na Waislam.
Naamini Rais Hussein Mwinyi anatambua dhima anayobeba mbele ya Allah na mbele ya nduguze Wazanzibar wanaomkaribisha katika misikiti yao wakanyanyua mikono yao juu kwa Allah kumuombea yeye dua na kuiombea Zanzibar salama.
Wazanzibari hawategemei baada ya haya yote damu ya Mzanzibari itakuja mwagika bila haki kwa sababu yoyote ile na yeye yupo madarakani.
Utakuwa msiba mkubwa.
Hakika Wazanzibari kwa dua zao hizi mbele ya Allah wamemtwisha rais wao mzigo mkubwa sana.