Wazanzibari ni wazalendo wa nchi yao ila Watanganyika sijui tuna matatizo gani!

Wazanzibari ni wazalendo wa nchi yao ila Watanganyika sijui tuna matatizo gani!

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Huyu mbunge ameongea jambo la maana sana juu ya mstakabali wa nchi yake ya Zanzibar ila alicho ambulia mitandao ni matusi, kebehi na dharau juu yake na kwa Wazanzibari kutoka kwa Watanganyika(Watanzania).

Screenshot_20240424-093459.jpg

Ni nini huko somo la uraia linafanya mashuleni juu ya Watanganyika mbona ni wapumbavu hivi wasiojali lolote kuhusu umuhimu na uhai wa nchi yao.

Nachoona ni Wazanzibari kuipigania na kujivunia Zanzibar kadili wawezavyo ila kwa Watanganyika hata tu nchi yao na utambulisho wao hawataki hata kuusikia.

Nampa heko huyu mbunge.

Bunge lilipaswa kuchafuka hoja za uhai wa nchi ya Tanganyika katika kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile.

Watanganyika wamerogwa ? Au nini?

Nyerere aliwafanya nini Watanganyika?

Pia soma: Mohamed Issa: Wanaotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar wawe na Passport
 
Nafikiri Elimu ya kujitambua ndio tatizo kwa raia wengi wa Tanganyika.
Ni Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila tu peke yake ndiye ambaye ktk maisha yangu ya hapa duniani nimewahi kumfahamu fika kabisa kwamba alikuwa anajitambua, mzalendo halisi wa nchi yake ya Tanganyika na pia ndiye aliyekuwa kinara mkubwa ktk kupigania haki na maslahi ya nchi yake ya Tanganyika. Lakini kwa bahati mbaya kabisa isivyotarajiwa WADHALIMU walimwelewa vibaya na kumtafsiri ndivyo sivyo.

RIP Shujaa Mchungaji Christopher Mtikila.

RIP Dkt. Sengondo Mvungi.

RIP Prof. Juan Mwaikusa.
 
Huyu mbunge ameongea jambo la maana sana juu ya mstakabali wa nchi yake ya Zanzibar ila alicho ambulia mitandao ni matusi, kebehi na dharau juu yake na kwa Wazanzibari kutoka kwa Watanganyika(Watanzania).View attachment 2972416

Ni nini huko somo la uraia linafanya mashuleni juu ya Watanganyika mbona ni wapumbavu hivi wasiojali lolote kuhusu umuhimu na uhai wa nchi yao.

Nacho ona ni Wazanzibari kuipigania na kujivunia Zanzibar kadili wawezavyo ila kwa Watanganyika hata tu nchi yao na utambulisho wao hawataki hata kuusikia.

Nampa heko huyu mbunge.

Bunge lilipaswa kuchafuka hoja za uhai wa nchi ya Tanganyika katika kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile.

Watanganyika wamerogwa ? Au nini ?

Nyerere aliwafanya nini Watanganyika ?
Swali uzalendo ni nini? Kigezo kipi kimekufanya kusema Watanganyika siyo wazalendo kuliko watu wazanzibari? Uzalendo wao ni upi?
 
Back
Top Bottom