Wazanzibari tumemchoka Hussein Mwinyi

Wazanzibari tumemchoka Hussein Mwinyi

Inapendeza sana
Kama hakuna mwenye kauli ya kuwatetea wenyeji, hakuna fukwe itakuwa ya Umma.

Fukwe zote zitamilikiwa na Wageni

Nina wasiwasi hata pale Forodhani wanapoogelea wale Vijana huku wakichukuliwa video, panaweza kutwaliwa na Wageni soon

Maana naona kuna mgeni mmoja ameanzisha Mgahawa unaoelea pale (the floating restaurant)
 
Zanzibar mnataka nchi yenu iwe kama Dubai hakuna budi kujiandaa na mabadiliko ya kufukuzwa kwenye maeneo yenu...
Mwisho wa siku mtakuwa wakimbizi Tu
Acheni chokochoko na upotoshaji. Majengo yamechoka, mengine yamepasuka nyufa, yameshakaa miaka 50! Wanaohamishwa wanapewa pesa kwenda kupanga kwengine. Majengo yakiisha wote wanarudi na wengine wengi wanapata nafasi.
 
Tangazo jipya la kuwaondosha zaidi ya familia mia tano katika mtaa wa kikwajuni kwa kuwapa wawekezaji ni kitendo kisicho kubalika kabisa.
Tangu alipoapishwa kuwa raisi, Mwinyi amekuwa ni kitendawili kwa jamii yetu. Fukwe za bahari zote zimepewa wawekezaji kwa kujenga mahoteli ya kitalii. Mitaa na wanachi wameondoshwa makwao kupisha ujenzi wa Mwinyi na watu wake. Sisi tuna uwanja wa ndege kisauni sasa kuna taarifa ya kujenga kiwanja cha ndege chengine. Hiyo nafasi iko wapi?. Hizi ardhi zetu munasema ni za serikali mbona munawapa watu wasiokuwa na hisia ya ardhi zetu. Mwinyi kweli ametimiza ambayo wenzake walishindwa kutekeleza.
Tunawaomba CCM muje muchukuwa pandikizi lenu. Sisi tumechoka nae. Yeye anajuwa kuwa hapati kura kwa hiyo CCM itambeba kwa hali yoyote ile.
Kwani Mwinyi sio Mzanzibar?
 
Screenshot_20241103_083516_X.jpg
 
Anataka mkajae Tanganyika, kisha mjimilikishe na mseme ni Nchi yenu.
Mwenzenu anataka wote mtoke huko muwe mnaenda kutalii kama Wamasai wa Ngorongoro.
 
Kama hakuna mwenye kauli ya kuwatetea wenyeji, hakuna fukwe itakuwa ya Umma.

Fukwe zote zitamilikiwa na Wageni

Nina wasiwasi hata pale Forodhani wanapoogelea wale Vijana huku wakichukuliwa video, panaweza kutwaliwa na Wageni soon

Maana naona kuna mgeni mmoja ameanzisha Mgahawa unaoelea pale (the floating restaurant)
Forodhani ni sehemu ya eneo la hifadhi ya Mji Mkongwe (Stone Town), wale vijana na wafanyabiashara wanaruhusiwa kama sehemu ya burudani kwa watalii
 
Okay, bora iwe hivyo maana Wanasiasa wetu hawachelewi kuuza Kwa Wageni hayo maeneo
 
Back
Top Bottom