wazanzibari watofautiana juu ya tathmini ya Warioba


chabuso;
hakuna anayeutaka muungano huu tena. Wenye muungano walishaanza kudhulumiana. Mara mafuta ni yangu lakini pesa za utalii wa kuuona mlima kilimanjaro na mbuga za wanyama ni zetu, mara nataka ukikopa ulete tugawane pasu pasu, huu ni muungano au ni kulishana halua???
Kama tumeungana kweli kweli, iweje weye uje bara kama waenda bafuni tu huulizwi chochote ila mie nikija kwenu wanisachi ka jambazi? Iweje weye ujiendee popote pale bara uchague mahala pa kuishi ila miye nikija kwako hata kama nina undugu nawe bado uninyanyase? Tanganyika tumewakosea nini?
Bora muungano mumeuvunja wenyewe wala sio Tanganyika. Fikiria, watu wasivyo na haya; wanakuja kutunga katiba ya JMT wakati wanajua wazi hakuna ya Tanganyika. Ili iweje? Mbona tayari mnayo ya Zanziba?? Si muulize ya wenzetu ii wapi??
Hatujasema muungano ukivunjika msikanyage Tanganyika, No no nooo. Mtakuja kama mnavyoingia Mombasa vile. Kinacho hitajika kule na huku ndivyo kitahitajika. Tunachohitaji sisi Tanganyika kuingia Kenya ni hicho hicho tunahitaji kuingia Zanziba leo. Mtazoea tu. Hatujasema kuwa tutawafukuza wake zetu huku wenye asili ya huko ila tutawahitaji wajue kuwa wana Taifa lao. Si umesikia habari za uraia wa taifa 2 hakuna hata humo mwenye hiyo Katiba mpya? Kaka, moto huu ni mkali mno kuliko tunavyo fikiria.
 
Bora huo muungano uvunjike waznzibar wabakie na Dubai yao nasisi tubakie kwetu ni kweli mtanganyika akifika znz utasachiwa utaambiwa hujui kiswahili utaitwa chogo wamesahau kama chimbuko lao Tanganyika tena wengi wamakonde na wanyamwezi minachoka sana wanavyojiona wamanga
 

we mpemba kama unakujaga Tanganyika kuzurura ndio uanze kujipanga. safari ya kurudi kibanda maiti imewadia. beba kila unachoweza mapema
 

Kaka mimi nakumbuka wakati wa Nyerere ambae ni muasisi wa mungano huu watanganyika walikuwa wanaingia kwa passport zanzibar na wazanzibar walikuwa wanaingia Tanganyika kwa passport pia,hali hiyo imeondolewa sio zamani sana,Salimini Amour ambae alikuwa raisi wa zanzibar kwa wakati huo pamoja ndio waliondoa hali ya kutembeleana kwa pasi...wakati wa Nyerere kama mhalifu kafanya uhalifu bara akikimbilia zanziabr basi polisi wa bara walikuwa hawana mamlaka ya kumkamata mhalifu huyo,na ilkuwa hivyohivyo kama mhalifu katoka Zenji kukimbilia bara,kwahiyo hayo unayoyasema sio mageni katika mungano huu wa wajanja, unaonyesha wewe bado mdogo sana hata huu mungano wenyewe huujui......,unaongea kutokana stori za vijiweni

wewe unavyooshesha sio mtembezi sana kati ya zanzibar na Tanganyika kero kubwa ya ambayo wazanzibari nimewasikia kulalamika ni pale ambapo mtu katoka zanzibar na kifuko chake lakiniakifika bandari ya daresalam natakiwa alipe kodi ya mapato mbona mtanzania akitoka Arusha kwenda Tanga mzigo haukatiwi kodi

Mkuu mimi na wewe ni wahanga tu wa huu mungano usiofahamika wanaofaidika na mungano huu ni wachache sana,usiwe
na jazba Mkuu, kwa Upande wangu nataka huu mungano uvunjike kila mtu achukue chake,kama kitu kimeishi kwa miaka 50 bado watu wanalalamika basi hicho kitu hakina maslahi,,,,,
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda nisaidie,Je Zanzibar ni nchi? Tafakari jibu lako ulilotoa bungeni Dodoma uchukue hatua.
 

chabuso,
umesema mengi sana lakini hili la kuniita tena mtoto naogopa kabisa. Miye simo miongoni mwa wale ambao hujifanya wazee vijana. Muungano ukiasisiwa miye nipo pale uanjani. Tena mtu mzima nikisoma pale Kinondoni Primary, Jeshi linaasi miye nipo shuleni tunakimbizana na wanajeshi wakipora vitu. Leo uniambie siujui muungano?? Kitu cha msingi ulichokisema hapa ni kuwa huu muungano wa sasa ni wa wajanjawajanja tu umebaki.
Waasisi wenyewe walidhani watanzania watajauamini kumbe ndiyo wanazidi kuukataa. Tangu lini Rais wa Muungano asiwe na mamlaka ya Zanziba? Ashindwe kuamua lolote mpaka amwulize wa Zanziba? Wa Tanganyika atampata wapi ili amwulize?
Jamani wauvunje tu kama tunaona vipi tukae chini tuangalie faida na hasara tukiona vipi turudiane. Wameshindwa wenyewe kuelewana, gari umenunua Zanzibar, unafika Darisalama unalipishwa ka umeinunua Dubai?? Umeona wapi hayo. Nchi moja, mamlaka tofauti. Huu ni muungano au usanii? Kama wanautaka uwe nchi moja, mikoa 28. Visiwani 2. Tutapona sivyo hakuna muungano hata wakitulewesha kwa siasa zao. Watu wameamka.
 
Undugu gani unaouzungumzia?kama ni undugu Afrika wote tu ndugu na makabila mengi yameingiliana,undugu utaendelea kama ambavyo waganda ni ndugu zetu,kama ambavyo warundi ni ndugu zetu,kama ambavyo wasudani ni ndugu zetu,undugu ambao hatutaki ni ule wa kubembelezana na watu ambao kila siku wanalalamika mara hiki mara kile,undugu wa mimi nikikufanyia ni sawa,lakini wewe ukinifanyia sio sawa,undugu wa chako chetu-changu changu,sasa huo ni undugu wa aina gani?si bora ufe tu?
 

Mtu ukiitwa mzanzibar elewa akili yako ka samaki, siku zote wanapiga kelele Tanganyika inawanyonya sasa kama kweli wanaupenda muungano kwa nini isiwe nchi moja na serikali moja ? wapuuzi hawa
 
Mkuu punguza jazba,wewe inaomyesha unatoka bara ya mbali sana ndio maana hujui undungu uliopo kati ya makabila ya pembezoni ya pwani ya afrika mashariki na wazanzibari,washwahili wamesema 'asiejua maana haambiwi maana' 😉

Muungano huu wakizungumkutu bora uvunjike lakini ndugu tutakuwa ndugu tu,wewe wabara utakuwa na ndugu zako wa uganda,Rwanda.....
 

naomba nikukosewe kidogo,Tanzania sio nchi moja, Tanzania ni nchi mbili zilizoungana yaani Tanganyika na Tanzibar.,Hizi nchi ziliungana kwa mashart 11 tu........

Hayo maswali uliyouliza ndio yamewafanya wazanzibar waomebe nchi yao,Na watanganyika waamke kisiasa,maswali watanzania walitakiwa wamuliza Nyerere na Karume kwani wao ndio walioleta haya mashaka.

wanaofaidika na mungano wako Oyester bay na Mbezi beach ,kwa upande wazanzibar wako mazizini

Binafsi mungano uvunjike sasa hivi,ukivunjika usivunjika sina hasara....Kitu kinachonishangaza mimi ni kuona watanzania wamenavyopelekeshwa kimawazo bila ya kufikiri.....
 

Huu ni uongo tu na unafiki
tu
Haohao ndo hawataki muungano sema hawataki kujulikana na ndo maana wanataka kura ya siri.
 
Jifunze kiswahili vizuri..ni maana ya neno "Vibari" sema vibali..-------...mnatuhitaji wazanzibari kwa kiswahili fasaha...Bila ya sisi kiswahili kwisha......
 
usitoke nje ya
mada wachina wanatumia vibari maalum kuishi tanganyika na nyie itabidi
mtumie work permit au visa kama wachina mjiandae haya mambo
yanakuja.

Kwani wachina wamepata wapi vibali vya kuishi tanganyika ata wazanzibar wavikose? Je wazanzibar walioko nch nyengne dunian wameweza kupataje vibali vya huko ata vya MRIMA wavikose?
 
Hakuna ujinga mkubwa unaofanywa km ujinga wetu ss watanzania mnaoomba muungano wetu uvunjike wote ni wapumbavu na sijawahi kuona watu wa aina yenu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…