Kaka kwa comment yako hii inaonekana unatoka bara ya mbali hapa Tanzania,kwa taarifa yako makabila kama wazaramo,wandengereko,wandengereko,wanyamwezi wameishi zanzibar miaka mingi tu zaidi ya miaka 100 au tangu walikuwa wageni mpaka wamezaana wamekuwa wenyeji wanasonga mbele..........
Wazanzibari sio kuwa wanataka kuvunja muungano ili wakosane na ndungu zao wa Tanganyika hapana kinachotakiwa na wazanzibar mungano wa kisaisa baina ya Tanganyika na Zanzibar usiwepo lakini muungano wa kiundugu utabakia pale pale hamna atakae weza kuuvunja,kumbuka kabla huu mungano wa kisiasa ulioletwa na Karume pamoja na Nyerere watu wa mataifa haya mawili ya walikuwa wamekusha ungana kindugu,
mfano Ali Hassan Mwinyi kabla ya mapinduzi aliekuwa raisi wa Tanzania alikwenda Zanzibar kusoma Madrasa 'Kuran' lakini mwishowe amefikia kuwa raisi wa zanzibar,hii inaonyesha hakuna chuki kati ya wazanzibari na ndugu zao watanganyika isipokuwa siasa uchwara za watu wachache zimeleta chuki baina ya wazanzibari na watanganyika.....
Binafsi naona huu mungano wa Nyerere na karume bora uvunjike kwani umeleta chuki baina ya ndugu wawili,kuvunja mungano isiwe chuki Mkuu,kichukulie kama kitu cha busara.....
chabuso;
hakuna anayeutaka muungano huu tena. Wenye muungano walishaanza kudhulumiana. Mara mafuta ni yangu lakini pesa za utalii wa kuuona mlima kilimanjaro na mbuga za wanyama ni zetu, mara nataka ukikopa ulete tugawane pasu pasu, huu ni muungano au ni kulishana halua???
Kama tumeungana kweli kweli, iweje weye uje bara kama waenda bafuni tu huulizwi chochote ila mie nikija kwenu wanisachi ka jambazi? Iweje weye ujiendee popote pale bara uchague mahala pa kuishi ila miye nikija kwako hata kama nina undugu nawe bado uninyanyase? Tanganyika tumewakosea nini?
Bora muungano mumeuvunja wenyewe wala sio Tanganyika. Fikiria, watu wasivyo na haya; wanakuja kutunga katiba ya JMT wakati wanajua wazi hakuna ya Tanganyika. Ili iweje? Mbona tayari mnayo ya Zanziba?? Si muulize ya wenzetu ii wapi??
Hatujasema muungano ukivunjika msikanyage Tanganyika, No no nooo. Mtakuja kama mnavyoingia Mombasa vile. Kinacho hitajika kule na huku ndivyo kitahitajika. Tunachohitaji sisi Tanganyika kuingia Kenya ni hicho hicho tunahitaji kuingia Zanziba leo. Mtazoea tu. Hatujasema kuwa tutawafukuza wake zetu huku wenye asili ya huko ila tutawahitaji wajue kuwa wana Taifa lao. Si umesikia habari za uraia wa taifa 2 hakuna hata humo mwenye hiyo Katiba mpya? Kaka, moto huu ni mkali mno kuliko tunavyo fikiria.