Nkazahau,
Mkuu maelezo yako murwa kabisa isipokuwa tu nawe unapindisha sana kuingia ktk Muungano wakati wenye matatizo ni sisi.
Nikisoma malalamiko yako yote hayaelezi kile unachokitaka wala mapungufu ktk Muungano. Nchi ikiwa na serikali moja, mbili au tatu haiwezi kuleta matatizo ikiwa sisi wenyewe tumejipanga vizuri na kuna makubaliano ya kimsingi..
Mkuu mimi ni "back bencher" kwenye mijadala ya JF na napenda kupata maoni ya wenzangu na nini wanakifikiria kwenye masuala mbali mbali yanayotukabili. Sasa wakati mwengine nashindwa kujizuia kujibu hoja zisizo na macho ndio maana sio rahisi kuona nini ninakitaka kwani huwa najibu hoja tu na kujaribu kutikisha fikra za wenzangu ili tupate kuelewa haya mambo kwa kina.
Kuhusu ninachokitaka mimi kwa sasa ni serikali tatu au mbili, hizi mbili moja ya Tanganyika na nyengine ya Zanzibar halafu tunaangalia maarifa ya kwenda kwenye East African Union 🙂, maana hapa East Africa sisi ndio wenye uzoefu wa muungano na tutasaidia sana katika kuimarisha muungano wa EAU. Na kama tumenufaika na muungano wetu basi inabidi tuwagawie ndugu zetu (wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi) hii neema tusiwe wachoyo.
Matatizo ya mgawanyiko wa wazanzibari ni ya kihistoria na sio rahisi kwa kiongozi mmoja au wawili kusimama jukwaani kulikemea hili halafu tukategema "miracle", kunatakikana mikakati mizuri na kila upande unaohusika au kila raia aelewe athari ya haya yanayoendelea sasa na kuwa tayari kuweka pembeni tofauti zetu, ni hapo tu ndipo tutakapokuwa na umoja wa kweli, matokeo ya hivi karibuni ni mwanzo mzuri lakini "we have a long way to go".
Kuhusu mapungufu ya muungano nadhani kama unafuatilia threads za JF basi ni mengi tu na ndio maana mimi kama raia naona kabla ya kuwa na informed opinion nilikuwa na hamu kubwa ya kuyajua makubaliano na hasa kuiona hii hati ya makubaliano, nishachoka kuwasikiliza baba, babu wajomba na shangazi etc wakifanya opinions zao kuwa ni facts.