Mkandara said:Matatizo ya ndani tu yanawashinda kuyaweka wazi na kuwalaumu vviongozi wahusika badala yake wanatumia UNAFIKI kutafuta mchawi toka bara na sii visiwani.
Mkuu ndio maana nikasema inabidi kwanza umwelewe Salim alikuwa akizungumza kitu gani..Mkandara,
..hicho ulichokiandika hapo juu ndicho kilichopaswa kuwa maudhui makuu ya hotuba ya Salim Salim. siyo kuanza kudai Wazanzibari waungane kudai haki zao kwetu, wakati wao ndiyo wanaofaidika zaidi na huu Muungano.
si wamesema wanamafuta na hawataki ku share na bara
kinachotakiwa ni serikali moja
unguja mkoa na pemba mkoa
total population ya zanzibar ni sawa na mkoa wa kinondoni
lakini znz kuna raisi, mawaziri na viongozi kibao halafu kazi hamna...
lakini kama muungano huu wa znz wana rais halafu bara hawana haufai, wala serikali tatu no....
wakati umefika wa serikali moja au basi lakini haya mambo ya znz kila siku kusema sisi ndio tunawanyima maendeleo haiwezekani......
embu fikiria mwanza ni kubwa kuliko znz, ina watu wengi mara mbili ya znz, uchumi wake ni mkubwa kuliko znz lakini znz kuna wabung 50 na mwanza 13
halafu bado wanaonewa na bado kuna baraza la wawakilishi...
..Salim Salim naye amenyimwa haki gani ktk Muungano huu?
..wasitusumbue hawa.
..dawa ya kuondokana na kadhia hii ni kuvunja muungano.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuwa United States of Tanzania, hivyo hatuhitaji Rais 2. Rais ni 1 tuu kama USA.
Masatu,
..Wazanzibari wanadai wananyimwa haki lakini hawaishi kungangania huku Tanganyika.
..kama kweli Tanganyika na wa-Tanganyika wangekuwa wabaya kiasi hicho, na wanawanyima haki basi, wangeisha ondoka kurudi kwao.
..tena wanadai "Wazanzibari tuungane kudai haki zetu" sasa nini kinakufanya wewe uamini kwamba wao na sisi tu wamoja?
..unadai tuweke UTAIFA mbele, sasa of all the ppl Salim Salim kwenda kutoa kauli ile "Wazanzibari tuungane kudai haki zetu" hivi unaona ameweka utaifa mbele? au tunaotakiwa kuweka utaifa mbele na wa-Tanganyika tu?
..binafsi sioni ambacho Mtanganyika anaweza kukipata huko Zanzibar ambacho hawezi kukipata hapa Tanganyika. Mtanganyika hana maslahi yoyote yale na muungano huu.
..ni kweli kwamba wakubwa wa Ulaya wanasisitiza sana masuala ya muungano. lakini tukumbuke kwamba wana sababu zao.
..kabla ya Watanganyika kurukia tu mawazo ya wakubwa, tunapaswa kuchunguza faida wanazozipata wakubwa hao kwa kuungana.
..WATANGANYIKA TUNAPATA FAIDA GANI KWA KUUNGANA NA NCHI YENYE WATU WACHACHE, ENEO DOGO, NA RASILIMALI KIDUCHU, KAMA ZANZIBAR?
Jasusi,
..watu kama Masatu huwa nawapa "thank you" hata wakinitukana!!
..and I never reply in kind kwa matusi yao.
Nkazahau,
Mkuu maelezo yako murwa kabisa isipokuwa tu nawe unapindisha sana kuingia ktk Muungano wakati wenye matatizo ni sisi.
Nikisoma malalamiko yako yote hayaelezi kile unachokitaka wala mapungufu ktk Muungano. Nchi ikiwa na serikali moja, mbili au tatu haiwezi kuleta matatizo ikiwa sisi wenyewe tumejipanga vizuri na kuna makubaliano ya kimsingi..
Mkuu mimi ni "back bencher" kwenye mijadala ya JF na napenda kupata maoni ya wenzangu na nini wanakifikiria kwenye masuala mbali mbali yanayotukabili. Sasa wakati mwengine nashindwa kujizuia kujibu hoja zisizo na macho ndio maana sio rahisi kuona nini ninakitaka kwani huwa najibu hoja tu na kujaribu kutikisha fikra za wenzangu ili tupate kuelewa haya mambo kwa kina.
Kuhusu ninachokitaka mimi kwa sasa ni serikali tatu au mbili, hizi mbili moja ya Tanganyika na nyengine ya Zanzibar halafu tunaangalia maarifa ya kwenda kwenye East African Union 🙂, maana hapa East Africa sisi ndio wenye uzoefu wa muungano na tutasaidia sana katika kuimarisha muungano wa EAU. Na kama tumenufaika na muungano wetu basi inabidi tuwagawie ndugu zetu (wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi) hii neema tusiwe wachoyo.
Matatizo ya mgawanyiko wa wazanzibari ni ya kihistoria na sio rahisi kwa kiongozi mmoja au wawili kusimama jukwaani kulikemea hili halafu tukategema "miracle", kunatakikana mikakati mizuri na kila upande unaohusika au kila raia aelewe athari ya haya yanayoendelea sasa na kuwa tayari kuweka pembeni tofauti zetu, ni hapo tu ndipo tutakapokuwa na umoja wa kweli, matokeo ya hivi karibuni ni mwanzo mzuri lakini "we have a long way to go".
Kuhusu mapungufu ya muungano nadhani kama unafuatilia threads za JF basi ni mengi tu na ndio maana mimi kama raia naona kabla ya kuwa na informed opinion nilikuwa na hamu kubwa ya kuyajua makubaliano na hasa kuiona hii hati ya makubaliano, nishachoka kuwasikiliza baba, babu wajomba na shangazi etc wakifanya opinions zao kuwa ni facts.
Ametimiza angalau wajibu wake kwa jamii yake na Afrika.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
Ukweli utabakia pale pale kuwa Hawa ndugu zetu wengi wao hawajaenda shule ya ki magharibi.
Uwezo wa kutoka nje ya box inakuwa ndogo.
Hilo ndo tatizo. Mimi huwa nawafananisha na wa Pelestina!
Ngoja nikimbie kabla ya mawe kurushwa humu!
Nasitiza tena Dr Salim Ahmed Salim,leave us alone,we do not need you any more!leo hii ndiyo anaisema chuki Waznz baina yao?alikuwa wapi miaka yote ambapo yeye akiwa waziri mkuu na baadae waziri wa ulinzi akiwa mjumbe mwenye nguvu sana ndani ya NEC ya CCM aliyehudhuria vikao na wenzake kuwetenga baadhi ya waznz ndani ya serikali ya Nyerere na mzee Mwinyi!
Alifanya nini alipokuwa na vyeo vya ndani na vya kimataifa kuwawezesha waznz wenzake wasizidi kujitemga na kutengwa?leo hii kawekwa kando na siasa za kiimla za tz ndiyo anayaona haya?
Amuulize mzee Machano,Mbwelezeni,Duni,Maalim na wenzake ambao wamerudishwa nyuma sana na serikali kuu ikiwemo kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.kwa ufupi hata yeye Salim alishiriki kuweka tabaka la utengano kati ya waznz wenyewe!
Why sasa anaanza kuzisema kuhusu kutengena kwa waznz akiwa nje ya dimba,na alipokuwa ndani ya duara kama tu wenzake na yeye alishiriki kuwatenga waznz hasa wenye muonekano tofauti na yeye kimawazo!
Dr salim hukuwepo kwenye vikao vya CCM vilivyofanyika Karimjee hadi usiku wa manane na kuwavua madaraka akina Maalim kwa kisingizio cha "kuchafuka hali ya siasa znz?",Je sio hapo ambapo hasa wanzn walianza kujitenga kutokana na ukanda kwa kiwango cha kutisha?ulifanya nini?Mauaji ya wanachama wa CUF mwaka 2001 ulichukua hatua gani kuyasemea?Pumzika tu salama Dr wetu Salim Ahmed Salim
Salimu anaonyesha ukomavu wake kisiasa na nafikiri angetufaa sana kama angepewa nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania, labda angeweza kukemea ufisadi kuliko serikali tuliyo nayo sasa ambayo inakumbatia sana ufisadi au niseme ni sehemu ya ufisadi. Ni kweli tatizo la Wazanzibar ni kuwa na umoja na kuwa na sauti moja lakini tatizo lao ni kwamba kila mtu anashika lake halafu at the end of the day wanalaumu wanaburuzwa na Tanganyika (sikukosea kutoandika Tanzania).
Tiba