Ni true story wadau.
Hivi majuzi maeneo ya Misugwisugwi Picha ya Ndege , ndugu zetu Wazaramo walimkamata mwizi.
Panja huyo alikua ameiba godoro , baada ya kukamatwa alikiri kuiba.
Kilichofata HAWAKUMPIGA HATA KOFI !
Walimsakama kwa maneno makali , ikiwemo MATUSI , MASIMBULIZI , MISUTO, WAKAMNANGA , WAKAMZODOA , WAKAMTIA MASINGI , MINYANYAPAO, MISONYO.
Hadi mwizi kafa kwa maneno tu!
Kwa hili Wazaramo shkamooni .
hee iyo kali kwelikweli maneno yanamuua mtu? i wonder!
ladyfurahia hata nami nilipoipata habari hii , awali nilidhani malimwengu!
Nilipofatilia nikakuta ni true event occured !
zaramo shikamoo...
siamini kama kuna ukweli
mh! babu alimkomesha mbaya!Achana na wazaramo!
Kuna mdada alikwenda market ku-buy fish , muuzaji alikua mzee wa kizaramo, ktk chaguachagua ya samaki , mdada akamuuliza "Babu mbona huyu Ngisi katepeta hivi?"
Jibu ; - "ndiyo katepeta alikua shoga tangu baharini huyo!"
Tena kwa taarifa muda huu Clouds Fm through Power break fast wameusemea mkasa huu.