Baba Kisarii
JF-Expert Member
- May 7, 2024
- 1,844
- 3,089
Kati ya vitu vinavyowatia hofu waTanzania wengi wanaotamani kupanda mlima ni pale wanapoona sisi wazoefu na watu wa milima tunabeba Mibegi mikubwa kama inavyoonekana katika picha.
Wanadhani nao wakija huku watabebeshwa mibegi yao. Haiko hivyo!
Ukiamua kupanda mlima utakuwa na ka begi kadogo kenye wastani wa kilo 2 tu na hako bado unaweza kusaidiwa pale itakapohitajika kufanya hivyo. Kwa kawaida kila mgeni mmoja anahudumiwa na Team ya watu wasiopungua watano na wanaweza kuongezeka kulingana na njia,idadi ya siku na mfumo wa Kampuni inayokupandisha.
Wote hawa ni wa kazi gani? Ukiamua kupanda mwenyewe bila kuwa kwenye Group utakuwa na;
-Guide Mmoja
-Mpishi Mmoja
-Wapagazi kuanzia Watatu au Wanne.
Nini Majukumu yao?
GUIDE
-Huyu atakuongoza njiani na kukupa story kadha wa kadha kuhusu Mlima.
-Ana uzoefu wa kutosha kuhusu hali ya hewa mlimani
-Atahusika kukupangia Mwendo ili usichoke na uwe na mpangilio wa kupumua usiheme sana!
-Siku zote anatembea na Kibox cha huduma ya kwanza kwa ajili ya kukabili dharura yoyote ya kiafya kama itajitokeza.
-Huyu ndiye mpangaji wa ratiba yako nzima ya siku hadi utakapomaliza kupanda na kushuka.
-Guide ndiye mfariji wako mlimani ambaye mtapiga story nyingi sana za kimaisha.Hata kama umeacha mvurugano huko nyumbani,kazini mtashauriana ikiwa utaamua kumshirikisha!
MPISHI
Huyu atashughulika na mambo yote ya mapishi na maandalizi yake yote. Atahakikisha unapata milo yako mitatu mizuri kabisa kadiri ya mapendekezo yako na mifumo ya vyakula vya mlimani vinavyopangwa.
Kupitia yeye utajikuta unapata Chai ya Kitandani(Bed Tea) hata kama huna kawaida hiyo hapo nyumbani kwako. Kama Mzungu vile. Daadeki😆
Na wakati wa matembezi kutoka kambi moja kwenda nyingine anahakikisha amekufungia kitu cha kutafuna njiani ili kukuongezea nguvu na afya izidi kuimarika. Ana hekaheka huyu si kawaida.
WAPAGAZI
Hawa tunawaita Injini ya Kazi. Bila wao hakuna kinachofanyika. Nguo zako zote na vifaa vyako muhimu wanabeba wao Hicho chakula utakachokipata kutwa mara tatu wanabeba wao. Gesi za kupikia zinatua migongoni mwao kila siku hadi siku unashuka. Ukichelewa kufika kambini wanakufuata kukupiga jeki wewe na Guide wako.Hapa namaanisha hata kale ka begi kako kadogo kenye chupa ya maji tu bado watakabeba.
Mahali pa kulala (mahema) wanabeba wao ikiwa utachagua njia inayotumia Mahema. Yaani kila kitu kinafanywa na watu wengine. Kazi yako inabaki kuwa ni: Kula, Kutembea, Kulala.....Baaas!😆
Gharama ya kupanda mlima haizidi Tsh milioni 1.7
Mpaka hapo utashindwa kweli?😆😆