Wazazi hawakuelewana Mahari, Binti anataka atoroke Nyumbani aje kwangu

Wazazi hawakuelewana Mahari, Binti anataka atoroke Nyumbani aje kwangu

Sio kweli Kuna time wazazi huwa wanawachalewesha mabinti Kwa tamaa zao za kiboya tu mwishoe wanaharibikiwa na Maisha so Binti anajua anataka Nini kwenye maisha na kafanya maamuzi
Sawa
 
Wakuu, ushauri wenu ndio unahtajika sana
 
Wakuu
Mimi ni kijana wa umri wa kuoa (miaka kati ya 23-30),mwezi wa nane mwaka jana nilienda kuchumbua katika kijiji jirani,

Nilienda na mwenyeji wangu,NA zoezi la kuchumbia lilikamilika na kishika uchumba tuliacha Tsh.10,000(kwa wale wasukuma watakubaliana na mimi kuhusu mchakato wa kuchumbia),

Badae wazazi wangu na wa mchumba wangu wakakutana kupanga mahari,lakini kiukweli hawakuelewana,wazazi wa binti walisema ng'ombe 12 lakini wazazi wangu walisema ni milioni mbili na laki mbili tu,hivyo hawakuelewana na wakapotezeana.

Lakini binti akazisaka namba zangu mpaka akazipata, tukawa tunawasiliana,anasema ananipenda na anataka tuoane tu licha ya wazazi kutoelewana,anataka kutoroka nyumbani kwao aje kwetu kuolewa,licha ya kumchenga chenga kuwa asubili lakini imefikia hatua binti analia anasema anakuja.
Na nikikataa atajinyonga

Mwishowe nikashawishika, akaniambia nimtumie hela ya kuja kwetu,ndo juzi nimemtumia elfu kumi atoroke aje kwetu

Wajuvi wa mambo mnanishauri/mnanisaidia vipi katika hili?

Karibuni.
Mtego huo kama ng'ombe 12 umeshindwa hapo utakutana na kitu kizito zaidi ya ikooo mkuu
 
Back
Top Bottom