Wazazi hawana aibu ndio maana watoto hawana adabu

haszu

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2017
Posts
978
Reaction score
2,313
Mtu akisha kosa aibu anaweza fanya au ongea jambo lolote lile.

1. Ilikuwa ni aibu kwa wazazi kuozesha binti yao na akawa sio bikra, now si aibu.

2. Ilikuwa ni aibu mtoto kuzalia nyumbani bila ndoa sasa si aibu tena.

3. Ilikuwa ni aibu kwa wazazi kupokea mali yoyote kwa mtoto wao bila kujua imetoka wapi, si aibu tena.

4. Wazazi wa sasa uzungu mwingi kuvaa vipenzi, kupost pucha za ajabu n.k

5. Wazazi hawana aibu kugombana mbele za watoto nk.

Kifupi haya(aibu) imetoweka katika jamii ndio maana adabu pia inatoweka.

Adabu na Haya zianaenda sambamba. Mtu aliekosa Haya hawezi kua na adabu kamwe.
 
Tracking ya kizazi cha hovyo kilianzia miaka ya 80's hawa ndio walisambaza ukimwi sana , hawa ndio wamezaa hawa Gen-z ....Mabalaa kibao wameleta .
 
Siku hizi ujinga na confidence vinaenda pamoja,
Ndio tatizo kubwa.
 
Uzi kama huu wachangiaji wachache leta uzi wa kula tunda sasa wachangiaji kama wote.
Dunia imebadilika mkuu

Wimbo wa Twenty percent Tamaa mbaya unasikilizwa na wachache tu.

Sasa rejea Komasava challenge kila mahali
 

No. Ilikuwa aibu pia kwa mtu mzima (mwenye umri wa kuwa mzazi) kuwaangalia tu watoto wakifanya mambo ya aibu bila kuchukua hatua.

No. Jamii nzima ilikuwa ikiona aibu kufumbia macho mambo ya aibu yakitendeka.
 
Kama taifa tu kuumiza wananchi wake halioni aibu....sisi aibu tutoe wapi!? We huogopi!?
 
no. 1 na 2 mzazi hawezi kuzuia, asali tu.

labda sijui afanye nini.
Umenena mkuu.
Kumzuia mtoto asitolewe bk kabla ya ndoa ama asipate mimba aisee wewe sali tu kwa Mungu.
Maana wengine wanabanwa mabinam wanawatunga mimba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…