Wazazi je tunaongea na wanetu?

Wazazi je tunaongea na wanetu?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Posts
4,219
Reaction score
4,608
nasisitiza wazazi tuongee na wenetu jaman
tuache kukumbatia mila na desturi
zinazotungamiza jana nipo kwenye dala dala
natokea kimara kwenda kkoo watoto wa
shule wamepanda wakaka seta ya nyuma
wakati wanashuka wakampa konda hela
konda akawakata hela ya mtu mzima wakati
wamevaa uniform wakaanza kusema si
wanafuzni konda kasema na mlivyokaa
mmoja akaanza kulia driver katia uyo wa
nyuma mzuri usichukue hela yake akupe
number ya simu nkiwaangalia wapo form
one au two kakawa kanacheka cheka na
konda anamrudishia nauli me nipo seat ya
mbele nkampa konda mia 5 na kuwaambia
shukeni si mmefika aliekuwa analia
akanyamaza wakashuka na ahsante nyingi
roho ikaniuma sikuwa na mda wa kukaa nao
niongee nao manake walikuwa wanawahi
shuleni sasa kwetu sisi wazazi kama
hatuongei nao nyumbai nani aongee nao?
konda?mwalimu?mpika chips?wanafunzi
wenzao?majirani zetu?akiambiwa na konda
ni mzuri kwanini asimpenda na hajawai
ambiwa na mtu yeyote?jaman wa kizazi
changu hao watoto tunaowakuza ni jukumu
letu tusikimbie haya majukumu ya kulea
watoto kuwapa right information kadri
wanavyokuwa waje wa make informed
decision tukimtegemea mwalimju wa science
kimu afundishe watoto zetu kwa dunia ya
saizi tutegeme mabaya zaidi ya yaliotukuta
 
hilo ni kweli na muhimu sana. Ila hekima inahitajika maana watoto wa siku hizi nao .... Mhhh ...
 
Ahsante sana kwa swalii zuri....

Hivi karibuni nilikuwa nafanya utafiti wa wazazi kukaa na watoto au vijana wao (nililenga zaidi teenagers) na huwezi kuamini nilichokipata, hakika ni aibu nikilinganisha na mzazi wangu alivyokuwa akitumia muda wa kutosha kukaa na kunipa life lessons nikiwa teen.

Nilichogundua ni kuwa (najua utashangaa) more than 85% hawajisumbui kukaa na watoto wao na ukisikia mzazi kakaa na mtoto wake basi ujue siku hiyo kapata story mtaani ya mtoto wake kafanya jambo baya hivyo sio tena session ya kumfunda mwanae bali ni session ya kumuadhibu mtoto kwa kosa alilofanya.....

Kuna tofauti kati ya hayo mawili na kuwa na muda binafsi na mtoto kunamjenga sana na kum-mold kuwa potential kwa siku zinazokuja

Tatizo ni kuwa wazazi wengi wanalalamika na kuongea sana juu za tabia za watoto wao lakini ukiwauliza wamewasaidiaje utasikia "mitoto ya siku hizi haisikii kabisa"
 
wazazi tunajiweka kwenye ubusy hatuamini kama tuna nafasi ya kuongea na watoto kila kitu tunategemea kuangalia diary na kupata mapokeo kutoka kwa walezi amabao ni walimu
 
Watoto wote siku hizi wana shida kubwa tu, wa kiume hajui roles za baba na wa kike halikadhalika! Msichana analaumiwa hajui kupika,wakati kalelewa na mama ambae akitoka kazini anapita mahali anapata kmoto na bia 3 anarudi home saa nne. Baba ndo hana hata taarifa za mkewe manake yeye anarudi saa saba!
Mfumo wa dunia unahitaji overhaul!

hahahahah sasa waki- overhaul staili ya maisha je ikisagika tena itakuwaje???
wengine wanaamini wana sababu za msingi kulingana na nature ya kazi na mahali wanapoishi (umbali) lakini naamini hata weekend kweli unakosa hata masaa 4 yakukaa na mtoto au hata kukaa nae mnaangalia TV walau ujue hata mtoto anabehave vipi??? na watoto wameamua kuishi kitamthiliya yaani hahahaha kazi ipo
 
unaongelea hawa wazazi wanaoondoka nyumbani sa kumi na moja asubuhi na kurudi saa nne usiku? Hawa wazazi ambao wamewaachia wasaidizi wa kazi malezi. Hawa wazazi wasiojua nini kinaendelea kwenye maisha ya watoto?
 
kweli kabisa

Funguka mkuu! Kweli kabisa nini? Changia mada!
Back to the topic:
Wazazi wengi wa siku hizi hawana muda na watoto wao, na hii husababisha kushuka kwa maadili!
 
Ahsante sana kwa swalii zuri....

Hivi karibuni nilikuwa nafanya utafiti wa wazazi kukaa na watoto au vijana wao (nililenga zaidi teenagers) na huwezi kuamini nilichokipata, hakika ni aibu nikilinganisha na mzazi wangu alivyokuwa akitumia muda wa kutosha kukaa na kunipa life lessons nikiwa teen.

Nilichogundua ni kuwa (najua utashangaa) more than 85% hawajisumbui kukaa na watoto wao na ukisikia mzazi kakaa na mtoto wake basi ujue siku hiyo kapata story mtaani ya mtoto wake kafanya jambo baya hivyo sio tena session ya kumfunda mwanae bali ni session ya kumuadhibu mtoto kwa kosa alilofanya.....

Kuna tofauti kati ya hayo mawili na kuwa na muda binafsi na mtoto kunamjenga sana na kum-mold kuwa potential kwa siku zinazokuja

Tatizo ni kuwa wazazi wengi wanalalamika na kuongea sana juu za tabia za watoto wao lakini ukiwauliza wamewasaidiaje utasikia "mitoto ya siku hizi haisikii kabisa"

I agree with you. Tuna (kwa sababu na mimi ni young parent) iachia TV set na cable vi replace mahusiano ya wazazi na watoto. Tunaona ni maendeleo mtoto/watoto kuwa glued mbele ya TV kwa masaa 8 kwa siku, na pia wazazi wengi wa hiki kizazi cha teknolojia tuna tabia mbaya sana ya kuhamishia ofisi nyumbani. Unakuta mzazi/wazazi hawana hata lisaa limoja la kuongea na watoto wao, au kucheza, kuimba nao, kama ni wadogo kuwasilikiza. Ok basi tuonyeshe at least interests na mambo wanayofanya, kama mtoto anaangalia show yake, why not join him/her? Baba yuko busy, mama yuko busy, siku, wiki, mwezi, mwaka unapita...before you know it wewe kama mzazi unakuwa si relevant tena kwa mwanao. Marafiki zake (peers) ndio wanakuwa na influence kwake on how to do things na wewe mzazi kwa sababu you were not there unakuwa source ya income tu.
 
Back
Top Bottom