Wazazi kuwaambatanisha watoto na Ibadan si ushamba!

Wazazi kuwaambatanisha watoto na Ibadan si ushamba!

Kimwakaleli

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2018
Posts
7,755
Reaction score
11,737
Habari Wana JF, Namshukuru sana Mungu kwa kumuweka hai,Katika hii Dunia kuna mambo mengi sana mazuri na mabaya, Moto huzaliwa na wazazi wake yaani Baba na mama,haijalishi atalelewa na Nani.

Kumetokea matukio mengi ya ajabu na yenye kutisha yanayotendwa na binadamu wenzetu,asilimia kuwa utagundua ni watu ambao katika makuzi Yao hawkufundishwa vizuri na wazazi wao mambo ya dini, Sunday school,misikitini ,nk Mfano makanisani nikiwa mdogo(Mithali 22:6)Mlee mtoto katika njia impasayo,naye hataiasha,hata atakapokuwa Mzee.Hii nimeishii hadi Leo Nina miaka54.

Huko tulikotoka kulikuwa na vyombo vya habari lakini si kwa Kasi ya Sasa, ambayo Dunia ni kama Kijiji.Kila mtu ni mdadisi na mwandishi wa habari,matukio yakitokea tayari yamejulikana kwa haraka sana.

Watoto wetu wafundishwe elimu Dunia lakini pia wafundishwe mambo ya dini ili wawe na Hofu ya Mungu hata kama watakana uwepo wa Mungu Bado Sheria za nchi zinaendana na maudhui ya dini Dini imetaja usiue,usiibe,usizini hakuna nchi inyoruhusu hayo pia Ahsanteni.
 
Haohao watu wa dini tena viongozi wa dini masheikh, mapadri na wachungaji ndio wabakaji na walawiti nambari moja wa watoto na wanawake huko kwenye nyumba za ibada.

Huhitaji dini ili kujua kwamba hupaswi kuua, kuiba n.k Mambo yote haya yanafundishika kwenye malezi kuanzia nyumbani.

Huhitaji kiongozi wa dini aje kumfundisha mwanao mambo haya, wewe kama mzazi unaweza kumfundisha mtoto wako mambo haya hukohuko nyumbani.

Dini ni kichaka cha madhalimu wala hakina mchango wowote ule kwenye malezi ya mtoto zaidi ya kumuharibu mtoto na kumwaminisha imani zisizo na msaada wowote ule kwake.
 
Umeeleweka ,ila inasaidia mkuu hao unawasema wengine ni watumia tumbo hata hiyo dini pia hawakufundishwa utoto !Kama umesoma vizuri maelezo yangu,ndivyo Mimi nilivyofunzwa na kuyaishi na hadi Sasa naishi hivyo,Mithali 22:6,Mlee mtoto katika njia impasayo,naye hataicha,hata atakapokuwa Mzee!Nina miaka 54 kwa Sasa Hilo fungu nilifundishwa 1979 nikiwa na miaka9,nyapu bila maelewano,Moja yangu haisimami!
 
Habari Wana JF, Namshukuru sana Mungu kwa kumuweka hai,Katika hii Dunia kuna mambo mengi sana mazuri na mabaya, Moto huzaliwa na wazazi wake yaani Baba na mama,haijalishi atalelewa na Nani.Kumetokea matukio mengi ya ajabu na yenye kutisha yanayotendwa na binadamu wenzetu,asilimia kuwa utagundua ni watu ambao katika makuzi Yao hawkufundishwa vizuri na wazazi wao mambo ya dini, Sunday school,misikitini ,nk Mfano makanisani nikiwa mdogo(Mithali 22:6)Mlee mtoto katika njia impasayo,naye hataiasha,hata atakapokuwa Mzee.Hii nimeishii hadi Leo Nina miaka54.Huko tulikotoka kulikuwa na vyombo vya habari lakini si kwa Kasi ya Sasa,ambayo Dunia ni kama Kijiji.Kila mtu ni mdadisi na mwandishi wa habari,matukio yakitokea tayari yamejulikana kwa haraka sana.Watoto wetu wafundishwe elimu Dunia lakini pia wafundishwe mambo ya dini ili wawe na Hofu ya Mungu hata kama watakana uwepo wa Mungu Bado Sheria za nchi zinaendana na maudhui ya dini Dini imetaja usiue,usiibe,usizini hakuna nchi inyoruhusu hayo pia Ahsanteni.
Ni ushauri tu
Acha nafasi au aya katika uandishi wako ili tuweze kusoma vizuri
 
Ni kweli kabisa mleta mada. Watoto wafundishwe mambo ya dini wakiwa wadogo. Pamoja na kwamba kumekuwa na matukio mengi mabaya huko huko kwenye dini, lakini bado inatupasa kuhakikisha watoto wetu wanapata mafundisho ya dini kwa lengo la kuwajengea imani, na misingi ya maisha. Kama mzazi unaona dini sio kipaumbele kwako na unauwezo wa kufundisha watoto wako wakapata mafundisho kiimani na kimisingi ya maisha ni nzuri pia. ila usiwaache watoto wafundishwe na dunia bila kuwajengea misingi kiimani na kimaisha kwa ujumla. Cha maana zaidi zichunguze hizo taasisi za dini kabla ya kupeleka watoto, fuatialia kila mafundisho yanayotolewa kwa mtoto wako. Kumbuka sisi ni binadamu na tunaishi katikati ya mbwa mwitu. Maarifa na akili za ziada zitumike..... think big ...
 
Umenena vyema mkuu,Dunia mambo yanayotendeka ni watu kukosa hofu ya Mungu!
 
Back
Top Bottom