awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa jamii forum kwa kuaccept usajili wangu. nimekuwa nikijaribu atleast kupost my opinions lakini kutokana na ugeni ktk matumizi ya teknolojia nikashindwa. Mi ni mkereketwa hasa ktk masuala ya elimu bcoz ni mwl niliyesoma ktk kipindi ambacho ethics za ualim zinatekelezwa ipasavyo.
Napenda kutoa maoni yangu juu ya matokeo ya kidato cha 4 kama ifuatavyo:
1- wanafunzi wa wakati huu kutokuwa na nidhamu, sifikiri kama pasipo na nidhamu kuna mafanikio ktk jambo lolote nidhamu ni jambo la msingi sana. malezi mabaya ya wazazi yanawajengea watoto wa leo kuwadharau walimu wao hivyo kudharau na kile wanachofundishwa.
2-matumizi mabaya ya teknolojia kama vile simu za mkononi, compyuta n.k. Wanafunzi hawatumii teknolojia kwa ajili ya kutafuta elimu bali kuiga mambo ya kipuuzi kama vile picha za ngono, mavazi ya kutuacha uchi kwa kudai kuwa ndo usasa.
3-walimu hawatoshelezi
4-kutofanya mtihani wa mchujo wa national form2, wanafunzi wanabweteka sn kusoma miaka minne mfululizo bila kipimo chochote hasa ukizingatia kuwa miaka ya hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakijiunga kidato cha 1 bila kujua kusoma wala kuandika. watendaji wa elimu mikoa na wilaya kulundika walimu shule za mijini na kusahau za vijijini.