Wazazi/mzazi wa binti


Leo shost umetuvalia njuga haswaa........haya na sie tusoijua Biblia? wenye dini tofauti ndo unasema tuhamie au? mwe! Caro leo umeniweza dadangu!! najuuuuuuta kukufahamu lol
 
Reactions: Mbu

.....wooowww,...finally umefunguka, na nimependa sana mchango wako wa mawazo...
ila kama nilivyoandika kwenye utangulizi, ----pamoja na mafundisho na muongozo wa kiroho;

utamuongoza/kumlinda/kumsaidia/ vipi binti wa chini ya miaka ishirini na moja kuepukana na vishawishi vya usasa
usipomnunulia wewe blackberry, atanunuliwa....

asipoangalia vipindi vya dstv kwako, ataangalizia kwa shangazi, mjomba baba mdogo nk, almuradi asiwe left out shuleni kwa wenzake...

utakabiliana nalo vipi hilo...kumbuka, NO pia inatakiwa ipatiwe ufafanuzi wake
...
 
CD shule yako imekuwa ngumu kidogo kuielewa hasa unapoongelea mtoto wa nje <br />
<br />
 
Reactions: Mbu
Tatizo kama mwanao ni chenga hata umfunge bango yataingilia kushoto na kutokea kulia,nakumbuka siku mzee anakaa na kutufunza hayo mambo ya ukubwa me nilisha ya master 3 yrs before,maza nae anajifanya kama askii yuko bize anasuka nywele
 
Reactions: Mbu
CD shule yako imekuwa ngumu kidogo kuielewa hasa unapoongelea mtoto wa nje<br />
<br />

Leo Dada Caro kaamua kutupa mitihani shost yaani mwe!!
Sasa hapo chukua mtoto wa nje, changanya na picha kuwa mnatoka dini tofauti......................unaanzia wapi?! sijui ndo uanze kwanza kuingia darasani kujifunza dini yake ndo mkae muelewane!! Eh, nahisi leo nikimuota Caro, sitashangaa kabisa!
 
Reactions: Mbu

Asante
Nimefurahi kwa hii topic ikanigusa kutaka kujua na upande wa pili couse unanihusu sana.........kupata mbinu zaidi na kuongeza maufundi pale ninapokwenda ndivyo sivyo........michango inayoendelea inazidi kunipa mwanya zaidi
..... thanx again
 

....lol....umeniibia password yangu wewe, nitakushtaki kwa moderator....ha hahaha...
 

....lol....umeniibia password yangu wewe, nitakushtaki kwa moderator....ha hahaha...

Eh Mbu we acha tu, yaani Caro leo kanikata maini kabisa! wala usinicheke!
I have been there, you know! and am telling you it aint easy kama ukisema unabase kwenye dini peke yake.
 
Reactions: Mbu
Vunja ukimya, zungumza na mwanao.
 
Reactions: Mbu
ndiyo hapo wazazi wanatamani binti yao asivuke umri wa miaka 7
 
Reactions: Mbu
Kusema ukweli malezi ni magumu na 'mazungumzo' kati ya mzazi/wazazi na mtoto yanapaswa kuanza mapema zaidi, Jana nilikuwa naangalia taarifa ya habari, mbabu wa miaka karibia 55, amepigwa kwa kumbaka mtoto wa miaka 9 ambaye mama yake alimtuma nyumbani kwa Mbabu huyo akaombe chumvi. Baada ya kukamatwa Mbabu anajitetea kuwa " Ni kweli nimemfanya, lakini sikumalizia!!! - meaning yeye hakufika kilele!! kwa kuwa watu walikuja kumvamia". nilishikwa na hacra na huzuni nikatamani yule mwandishi wa habari amzabe japo kibao. Nikaishia kujiuliza ina maana kuna watu leo hii hawajui kuwa hili ni kosa?

Lakini baadae nikawaza wazazi kama wazazi nafasi yetu ya kuwaandaa wenetu na hizi changamoto iko wapi? Je tumeshaweza kumfundisha mtoto 'dalili' na 'mbinu' na aina ya vishawishi ambavyo akiviona ajue hatari iliyopo mbele yake?? Sijui

Kwa hii mada ndo nachanganyikiwa kabisaaaa...........hivi sie wazazi, pamoja na 'uzoefu' wetu katika mapenzi, kweli tuna uwezo wa kuwaainishia wenetu, dalili ya mpenzi wa uwongo? tapeli? au ambaye ni likely kuja kumwuumiza huko mbele so that tumwambie awe extra care na flan kwani tunahisi si mkweli, hana mapenzi ya kweli au atamletea maumivu mbeleni??

Yaani leo kama kuniweza mmeniweza!
 
Reactions: Mbu
Vunja ukimya, zungumza na mwanao.

...unaanzaje anzaje sasa bana...? hebu yabainishe maswalki ya kuanzia either 1-5, au ?



...khaaaa, mwanajamiione hapa umemaliza kabisa....
harusini mara nyingi utawaona kina mama wanalia machozi,....
mzazi mwanaume utajikuta yeye anafakamia pombe kukata stimu, kwani anajua huko aendako binti huko....

hii mada nitaipanua wigo zaidi siku zijazo....lakini hali inatisha... kumtayarisha binti aje kuwa mke mwema, mama, mlezi...acheni nyie...acheni kabisa na maskhara eti malezi ya mtoto wa kike ni sawa na mtoto wa kiume....
 

Mkuu..kuna vitu viwili vya kuzingatia. Umri wa mtoto na uhuru/Haki za mtoto.

Kumlea mtoto katika mwenendo unaokubalika na familia siyo lazima kuingilia na kumnyima uhuru wake hasa pale anapokuwa umri wa ujana (miaka 15 au 16 na kuendeleaa). Kumbuka Ku-access online email account ya mtoto wa miaka 4 siyo sawa na ku-access email account ya mtoto wa miaka 16 au 18. Hivyo basi kuna umri ambazo ni lazima kila kitu kiwe monitored kama email, internet usage etc na kuna umri ambao lazima tumpe mtoto uhuru na haki ya kujiamulia. Mfano kwa watoto wadogo hadi umri wa kati tunaweza kitu kama Kids Email | Safe Email for Kids) ambayo email za mtoto zinapitia kwa parent hadi approve ndiyo zinakuwa delivered katika inbox ya mtoto..(bila mtoto kujua). Lakini kuna umri ambao itabidi tumwache mtoto afungue email anayotaka ni umri gani? inategemea na maisha ya familia na malezi.

Kumpa uhuru na haki siyo kwamba ndio tumwache .. La hasa..ni lazima tuwe nae bega kwa bega.. Kumbuka mtoto lazima ajue maisha yake ni maisha ya familia hivyo basi furaha yake ndiyo furaha ya familia na huzuni yake ni huzuni ya familia. Binafsi, nitakuwa radhi kumruhusu binti yangu awe na rafiki ya kiume (umri ukifika) lakini kwa uangalifu sana. Kwani nikiwa mwanaume najua jinsi wanaume wanavyokuwa waharibifu. na hasa hivi vi"boyz" vinaanza uharibifu bado vi-dogo.. uharibifu siyo lazima uwe physical sex intercourse.."Broken heart" ni uharibifu tosha...Wakati tunaruhusu mabinti wetu waingie kwenye Game lazima mabinti wajue uchungu na tamu ya mapenzi.. binti lazima ajue Huzuni yake ni balaa kwa familia.. Ni jinsi gani ya kumwelekeza huko ..hapo nadhani inategemea na malezi na ukaribu wa familia husika...

In short, controls zinategemea na umri wa mtoto kadri anavyokuwa kijana kitu kinachobaki ni ku-strengthen awareness kwa mtoto kuwa chochote anafanya ni kwa ajili ya familia na wala si kwa ajili yake binafsi. Kama ataleta furaha au huzuni ni kwa ajili ya familia nzima na wala si kitu binafsi, nadhani kwa njia hii mtoto au kijana atakuwa muwazi kwa wazazi..nasi wazazi tutaendelea kuwa "baneti kwa baneti au sambamba" kama maafande wangu walivyokuwa wanasema kule JKT mafinga.
 
Malezi siku hizi yamekuwa magumu sana, wazazi wenyewe mnawavalisha watoto wenu wa kike kama watu wazima, utakuta katoto ka kike kanene kamevaa kasketi hadi makalio yanaonekana, jiangalieni pia upya wazazi sababu dunia ilipofikia ni pabaya sana, utakuta zee zima linabaka mtoto wa miaka saba, waepusheni watoto wenu na mabalaa kwa kukaa nao na kuwaeleza umuhimu wa kujisitiri na yanayojiri sasa hivi mtaani
 
Good advice tulizo, kun a dada angu pia yuko over proctective kama nini sijui, mtoto wake sasa ana miaka 19 ana boyfriend, ssa kwa kumuogopa mama yake kaamua kushare na mie, na mie sitaki kuondoa ile trust nimwambie mama yake namwacha, ila kila nikikaa nae namwambia awe rafiki na mwanae atafaidi sana, coz atakuwa anashea nae vitu vingi sana
 
Reactions: Mbu

...dahhhh, hapa blackberry umenitolea mfano ulio hai kabisa.

1. umekubali malezi ya siku hizi yamekuwa magumu sana
2. unamlaumu dada yake amekuwa over protective.
3. una share secrets na "mpwa?" wako (mtoto wa dada)
4. hutaki/unaogopa kuvunja trust utapomwambia dada'ko
5. unashindwa ku link wawili hao....



...ipo siku litakulipukia....kabinti katasema aunty alikuwa anajua, dada mtu atakwambia kwanini hukumueleza mapema...
sasa jivishe 'viatu' vya dada'ko, utaanza anzaje kwenye umri huo ku interract nae?

1. ?
2. ?
3. ?
4. ?.....hebu tusaidie busara zako hapo, nawe utaona urahisi wa kumuelekeza dada'ko, kulikoni hivyo unavyomwambia juu juu "awe karibu na binti yake atafaidi sana...!" au nawewe una kauwoga kwa dada?
 
Nitarudi baadae...

MJ1 nimekumisi tu
Urudi Askofu utupe shuhuda za waumini wako.

Too bad sijaja kuungama muda mrefu Askofu. Nahisi siku nikija itabidi uwe na note book na kalamu! unawezasahau kunisamehesha mengine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…