Mkuu..kuna vitu viwili vya kuzingatia. Umri wa mtoto na uhuru/Haki za mtoto.
Kumlea mtoto katika mwenendo unaokubalika na familia siyo lazima kuingilia na kumnyima uhuru wake hasa pale anapokuwa umri wa ujana (miaka 15 au 16 na kuendeleaa). Kumbuka Ku-access online email account ya mtoto wa miaka 4 siyo sawa na ku-access email account ya mtoto wa miaka 16 au 18. Hivyo basi kuna umri ambazo ni lazima kila kitu kiwe monitored kama email, internet usage etc na kuna umri ambao lazima tumpe mtoto uhuru na haki ya kujiamulia. Mfano kwa watoto wadogo hadi umri wa kati tunaweza kitu kama
Kids Email | Safe Email for Kids) ambayo email za mtoto zinapitia kwa parent hadi approve ndiyo zinakuwa delivered katika inbox ya mtoto..(bila mtoto kujua). Lakini kuna umri ambao itabidi tumwache mtoto afungue email anayotaka ni umri gani? inategemea na maisha ya familia na malezi.
Kumpa uhuru na haki siyo kwamba ndio tumwache .. La hasa..ni lazima tuwe nae bega kwa bega.. Kumbuka mtoto lazima ajue maisha yake ni maisha ya familia hivyo basi furaha yake ndiyo furaha ya familia na huzuni yake ni huzuni ya familia. Binafsi, nitakuwa radhi kumruhusu binti yangu awe na rafiki ya kiume (umri ukifika) lakini kwa uangalifu sana. Kwani nikiwa mwanaume najua jinsi wanaume wanavyokuwa waharibifu. na hasa hivi vi"boyz" vinaanza uharibifu bado vi-dogo.. uharibifu siyo lazima uwe physical sex intercourse.."Broken heart" ni uharibifu tosha...Wakati tunaruhusu mabinti wetu waingie kwenye Game lazima mabinti wajue uchungu na tamu ya mapenzi.. binti lazima ajue Huzuni yake ni balaa kwa familia.. Ni jinsi gani ya kumwelekeza huko ..hapo nadhani inategemea na malezi na ukaribu wa familia husika...
In short, controls zinategemea na umri wa mtoto kadri anavyokuwa kijana kitu kinachobaki ni ku-strengthen awareness kwa mtoto kuwa chochote anafanya ni kwa ajili ya familia na wala si kwa ajili yake binafsi. Kama ataleta furaha au huzuni ni kwa ajili ya familia nzima na wala si kitu binafsi, nadhani kwa njia hii mtoto au kijana atakuwa muwazi kwa wazazi..nasi wazazi tutaendelea kuwa "baneti kwa baneti au sambamba" kama maafande wangu walivyokuwa wanasema kule JKT mafinga.