Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,861
- Thread starter
- #61
Thanks Mbu for the post..
Ndugu zangu, naamini chanzo cha tabia na mienendo watoto wetu hasa hawa mabinti ni sisi wazazi. Malezi ya tabia njema hayasubiri binti atimize miaka fulani kama 5, 10 au 18 ndiyo tukae naye chini.. that's too late. Kama umefanya hivyo hesabu maumivu...Kuna kitu inabidi mzazi ukishike kwa mtoto toka siku ya kwanza. Ni "bond" au moyo wa mtoto kwako..ukiweza kushika hapa..basi mtoto atakuwa vile wewe unataka... Lakini si kazi rahisi hata kidogo..kutokana na changamoto za maisha, ndoa, mapenzi, ubinafsi etc..
Mtoto huwa anazaliwa na asimilia 100% ya mapenzi na "bond" kwa walezi wake ambao mara nyingi ni wazazi. Ni sisi wazazi tunapunguza hiyo % kwa matendo na maisha yetu. Ili ku-maintain hiyo "bond" inabidi tujitoe muhanga katika maisha yetu na ubinafsi wetu. Inabidi tulee hii "bond" kwani haiji kirahisi kama mvua., hapo ndipo tunaweza kuonyesha mapenzi ya kweli kwa mabinti zetu toka wako wachanga hadi wanakuwa watu wazima. Hapo ndipo tutakuwa influential figure kwa maisha yao.. Hapo ndipo tuta-seal kiana watoto kusikiliza wapita njia na marafiki. Ni kazi ya miaka na ni maisha na siyo lele mama.
Maisha yetu ni elimu tosha kwa binti. Najua binti yangu ataniheshimu na kunisikiliza kutokana na maisha yangu na jinsi ninavyoonyesha kumjali toka yuko mchanga. Mapenzi na malezi siyo nidhamu ya woga. Siyo bakora hadi watoto wanakuita "Hitler".. Ni jinsi gani unaweza cheza na "feelings" za watoto hadi ukaweza ku-influence maisha yao. Ni vile wazazi tutakavyoweza ingia ndani ya mioyo ya watoto na kujenga fikra za mtoto za kuwa wao wana moyo nusu na nusu nyingine ya moyo wameshika wazazi. Ni vitendo vitajenga hii kitu na siyo maneno, darasa au ngoma ya unyago ya wiki moja. Ni mwenendo mzima wa maisha, nidhamu, upendo, mapenzi ya familia nzima. Familia inabidi iwe kitu kimoja mbele ya watoto hata kama kuna vitofauti kidogo chumbani…
In short, source ya mafanikio ya maisha ya mabinti zetu ni sisi wazazi. Maisha yetu na changamoto zetu, zi-depict vile tunataka maisha ya binti zetu yawe hivyo. Kwani matendo yanasema zaidi ya maneno. Ukipoteza hii opportunity ya kuwa influential figure ya mtoto ukategemea akikuwa mjomba au shangazi aje amfundishe au umpeleke kijijini akachezwe unyago basi ujue kama ni mtihani umeondoka na zero ya masikio.
dahhh tulizo wee....
post yako imejaa busara tele.
wazazi tuyasome na kujazingatia haya...bonding!