DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wazazi na walezi wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dabil, wilayani Babati, mkoa wa Manyara, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, ili kuwachagua viongozi wanaowataka kwa mujibu wa haki yao ya kikatiba.
Wito huo umetolewa wakati wa maadhimisho ya mahafali ya 20 ya shule hiyo, ambapo Afisa Elimu Kata ya Dabil, Cornel Silvin Mcharo, na Afisa Mtendaji wa Kata ya Dabil, Happiness Godfrey Sailale, waliwasisitiza wananchi kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia na kuwahimiza wanafunzi kujiepusha na vitendo vya kihalifu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Dabil, Haikasia Minja, amewataka wanafunzi wanaohitimu kuwa na nidhamu, kuheshimu mamlaka na viongozi wa nchi, pamoja na kujikita kwenye shughuli za ujasiriamali wakati wakisubiri matokeo yao.