Wazazi naombeni ushauri wa haraka jamani!

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2010
Posts
1,945
Reaction score
728
JF Doctor heri ya mwaka mpya!
Wakuu naombeni ushauri jamani ni kuwa siku ya mwaka mpya mke wangu alijifungua katoto ka kiume kakiwa na 4.5kg jambo lilioongeza furaha nyumbani ukichanganya na mwaka mpya.
Tatizo ni kuwa mke wangu hana maziwa kabisa toka ajifungue hata akijaribu kukamua hakitoki kitu jambo linalonishangaza kwa kuwa huyu ni mtoto wa pili na mtoto wa kwanza alimyonyesha vizuri tu.
Nimeshauriwa mtoto nimpatie maji ya uvuguvugu yenye sukari wakati namsubiria mama yake maziwa yaanze kutoka,nimeanza kumpa mtoto maji hayo toka jana lakini anakesha analia kwa kuwa hashibi kabisa na niliambiwa nisimpe maziwa eti utumbo wake bado mchanga.
Ndugu zangu naomba ushauri ni maziwa gani mbadala yanamfaa mtoto mchanga maana naona ananyongonyea pia naomba kujua njia za kusaidia mzazi kupata maziwa mbali na kunywa uji wa pilipili manga kwa wingi na supu ambavyo kwa sasa anatumia na havijatoa majibu mazuri.
Natanguliza shukrani.
 
pole mdau. JF Dk's where are u jamani. DR Riwa.. your help plz
 
Last edited by a moderator:
Huwa inachukua wiki moja hadi mbili mpaka mama aanze kutoa maziwa, na pia Kwa kuwa chuchu ni kubwa Mtoto anaweza asimudu ila lazima ivoivo awe anayakamua, anayakanda Kwa Maji ya moto Na mambo yatakuwa swari, ila mtoto apate ole laktogen 1 for the time being Na Maji Na uwe nae care sana aijepata manjano..ni hali ya kawaida hasa Kwa uzazi Wa kwanza
 
Consult wakina mama zetu co wapo wengi wamezaliwa na either kwa bahati mbaya mama kapendwa zaidi na Mungu na wakasurvive the storm so wao wana uziefu zaidi na daktari pia bila kusahau vyakula anavyo kula mkeo huchangia pakubwa kutengeneza maziwa niliskia vyakula vyenye nyanya kwa wajawazito kukata maziwa so fatutakitu mtori na vinginevyo vitasaidia..
 
Mtengenezee supu ya nyanya chungu (chemsha nyanya chungu za kutosha, weka kachumvi kidogo) waweza ongeza na viazi walau mviringo viwili anywe. Angalizo tumia nyanya chungu za kijani. Usitumie yale makubwa hayafai.
 
Mtoa mada ni hali ya kawaida mi ilinichukua siku tatu ndipo yakatoka ilinibidi nimpe lactogen 1 kuwa makini na kipimo soma maelekezo vizuri, anywe vitu vya moto na aendelee kuyakanda na kuyakamua yatatoka tu.
 
Mtengenezee supu ya nyanya chungu (chemsha nyanya chungu za kutosha, weka kachumvi kidogo) waweza ongeza na viazi walau mviringo viwili anywe. Angalizo tumia nyanya chungu za kijani. Usitumie yale makubwa hayafai.

Asante nimepata somo lingine
 
pole mdau. JF Dk's where are u jamani. DR Riwa.. your help plz

Dr.Riwa walimuudhi naona kagoma hata kuingia hata hivyo halimuhusu dr.kuna wazazi wazoefu humu.
 
Last edited by a moderator:
Wewe tafuta formular ya mtoto wa 0mwezi hadi 3 wakati unasubiri maziwa ya mama. Maji na sukari sio chakula!
 
Pole sana. Zaidi ya uji, supu na chai ya pilipili manga sijajua what else to do. Hebu nenda nae hospitali uongee na nurse yeyote yule, huwa wanajua jinsi ya kustimulate matiti kwa massage na maziwa yaanze kutoka.
Hongera sana.
 
Asante nimepata somo lingine

Nimewahi kusikia supu ya samaki aina ya Tasi pia husaidia kutoa maziwa, ukienda feri wapo wengi wanapatikana. Kingine ni supu ya kisamvu , I mean unatwanga kisha unachemsha na chumvi na pilipi kidogo, waweza tia na kitunguu bila nyanya mimi binafsi nimetumia hiyo na ilinisaisia. I had similar problem last year. try
 
anywe uji mwepesi aweke na pilipili mtama kwa wingi, ilimsaidia dada angu
 
Akoroge uji, aweke pilipili manga, kisha ukiiva changanya na maziwa mgando... ahakikishe anakunywa uji ukiwa bado wa moto...
 
Wakati mama anaendelea kutafuta maziwa, endelea kumpa mtoto lactogen 1, usipanic ni tatizo la kawaida mimi nina watoto wawili lakini wote hawakunyonya kabisa, afya zao bomba, ila jitahidi kuosha vizuri chupa na kuzichemsha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…