Mulangila Mukuru
JF-Expert Member
- Feb 24, 2010
- 1,945
- 728
JF Doctor heri ya mwaka mpya!
Wakuu naombeni ushauri jamani ni kuwa siku ya mwaka mpya mke wangu alijifungua katoto ka kiume kakiwa na 4.5kg jambo lilioongeza furaha nyumbani ukichanganya na mwaka mpya.
Tatizo ni kuwa mke wangu hana maziwa kabisa toka ajifungue hata akijaribu kukamua hakitoki kitu jambo linalonishangaza kwa kuwa huyu ni mtoto wa pili na mtoto wa kwanza alimyonyesha vizuri tu.
Nimeshauriwa mtoto nimpatie maji ya uvuguvugu yenye sukari wakati namsubiria mama yake maziwa yaanze kutoka,nimeanza kumpa mtoto maji hayo toka jana lakini anakesha analia kwa kuwa hashibi kabisa na niliambiwa nisimpe maziwa eti utumbo wake bado mchanga.
Ndugu zangu naomba ushauri ni maziwa gani mbadala yanamfaa mtoto mchanga maana naona ananyongonyea pia naomba kujua njia za kusaidia mzazi kupata maziwa mbali na kunywa uji wa pilipili manga kwa wingi na supu ambavyo kwa sasa anatumia na havijatoa majibu mazuri.
Natanguliza shukrani.