Wazazi ni chanzo cha ndoto nyingi za vijana kutokutimia

jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2013
Posts
5,352
Reaction score
9,329
Wakuu amani ya bwana iwe nanyi,

Kwanza kabisa hakuna mzazi hata mmoja ambaye anapenda mwanae au kijana wake asifanikiwe lakini kwa namna moja ama nyingine wazazi wamekuwa ni chanzo cha vijana na watoto wao kutokufanikiwa kwa maana ya kutimiza ndoto zao katika maisha,

Naamini sio mara moja au mbili umekutana na migogoro katika familia kwa sababu tu mtoto hataki kufanya kile wazazi wanachokitaka mfano wazazi wanataka mtoto asome masomo ya sayansi mtoto yeye anataka asome kitu kingine,

Mtoto anataka ajiajiri na sio kuajiriwa lakini hiyo inakuwa ni kesi nyumbani basi ndugu wataitana vikao na vikao wazazi hawataki kuelewa kuwa kijana wao ana maono ambayo huenda yakamfanya kuwa bora zaidi,

Kibaya zaidi huenda ajira yenyewe ndo hizi ikikatwa 60,000/= tu ni majanga,

Wazazi waacheni watoto wawe flexible bahati mbaya sana mnataka watoto wenu wafuate misingi ile ile mliyopita ilhali hakuna cha ziada mlichokifanya mpaka leo

Wazazi mpaka leo hamna uhuru wa kiuchumi bado mnafanya kazi maofisini tena kwa kupelekeshwa sometimes na vijana wadogo wanaofanana umri na watoto wenu lakini ninyi mnataka na vizazi vyenu viishi kama ninyi mlivyoishinkwa stress hata mkiombwa hela ya ada tu ya kawaida majanga

Wazazi waacheni watoto watimize ndoto zao wapeni full support ya watieni moyo

Nawasilisha

 
Dah huwa inauma sana. Unakuta Mzee Nyumbani ni Baba ila akifika kazini fullu kupelekeshwa na kutuma tumwa. mara nenda Benki, mara nenda TANESCO mara Idara ya Maji.
 
Dah huwa inauma sana. Unakuta Mzee Nyumbani ni Baba ila akifika kazini fullu kupelekeshwa na kutuma tumwa. mara nenda Benki, mara nenda TANESCO mara Idara ya Maji.
For sure lakini atafanya nini sasa wakati hiyo ndo kazi yake
 
Point kabisa. Ila vijana pia mjue sio kila jambo umueleze mzazi wako, unaonekana hujakomaa ndo maana wanapinga kirahisi.
Fanya mambo mengine kama surprise tu wataelewa mbele ya safari, ili mradi ujue unachokusimamia kwa moyo wa dhati na malengo dhabiti bila kukata tamaa hata nukta.
Watu wengi hawajui ukiwa umeajiriwa kufanya kaxi ya mtu maanake wewe huna Kazi. Na huo ndo ukweli wengi wanaupinga hata hawataki kuusikia.
 
Point kabisa. Ila vijana pia mjue sio kila jsmbo umueleze mzazi unaonekana hujakomaa ndo maana wanapinga kirahisi.
Fanya mambo mengine kama surprise tu wataelewa mbele ya safari ili mradi ujue unachokusimamia
Suprise? Hivi unajua ili kuzioatia movement zako inaweza kukuchukua hata miaka 10 mzee,

Yaani unaweza ukaanza kujenga brand yako au kampuni hata biashara ukaonekana bwege after 10 years watu ndo wakakuelewa

Hapo kweli unaweza fanya mambo kimya kimya bosi

Kwa sababu unapokuwa na vision haimaanishi utatoboa soon

Unapokuwa na vision means unawenza anguka mara nyingi sana kukamilisha plan yako na kuona mafanikio

Wazazi wanatakiwa wawe sehemu ya encouragment kwa wanao ili wawe na ile morali ya kufanya kazi

Mwambie mtoto ajipe moyo atafanikiw kwa kile anachokifanya

Kama inawezekana sometimes msaidie hata financially a-fund project zake

You never know bhana huenda akawa billionare baada ya miaka kadhaa

Unajua ukiwa unafanya kitu halafu unapata full support ya wazazi wako hata wengine wote wasipokuelewa ila mama na baba

Ukifail unajua nani wa kumueleza akutie moyo uwe na amani na upate nguvu za kusonga mbele

Wazazi wapeni nafasi watoto wenu watekeleze mawazo yao
 
Ni kweli, lakini ukitofautiana nao kimtazamo ufanyeje? Ufe kimya kimya au ujitusue.
Kwa familia zetu za afrika ni % ndogo sana ya wazazi wanaweza kumsupport mwana wao msomi kuwa mjasiliamali
 
Sure writer!

Katika maisha lazima uprove watu wrong,

Yaani wale wanaopinga idea zako lazima ifike hatua wakubali wapige salute,

Lakini ili pia umove vizuri lazima pia upate motisha kutok kwa watu wako wa karibu wanaokuamini

Yes watu hawa huwa kwanza kabisa ni wazazi wazazi wanacheza nafasi nzuri saka katika either kuboresha au kubomoa ndoto za mwanao

Umefika wakati sasa wazazi wacheze nafasi zao ipasavyo
 
Ni kweli, lakini ukitofautiana nao kimtazamo uufanye? Ufe kimya kimya au ujitusue.
Kwa familia zetu za afrika ni % ndogo sana ya wazazi wanaweza kumsupport mwana wao msomi kuwa mjasiliamali
Lazima ufanye mkuu ila ikikuchuchukua miaka kadhaa hapo ndo utaona dunia chungu

Ila kwa namna yeyote ile go for you Dream hata kama utabaki mwenyewe do it
 
Upo sawa. Tanzania mzazi yupo tyar kumsomesha mtoto wake india. Analipa million 10 kila mwaka. Miaka mi4 ni milion 40. Ila akimaliza chuo mzazi hawezi mpa hta m5 kma mtaji.
 
Upo sawa. Tanzania mzazi yupo tyar kumsomesha mtoto wake india. Analipa million 10 kila mwaka. Miaka mi4 ni milion 40. Ila akimaliza chuo mzazi hawezi mpa hta m5 kma mtaji.
Exactly mkuu

Basi kama hawezi kumpa mtaji amruhusu kwa moyo mkunjufu kufanya kile anachotaka kukifanya
Wazazi ndo wamekuwa wakikatisha tamaa wanao mpaka basi
 
Upo sawa. Tanzania mzazi yupo tyar kumsomesha mtoto wake india. Analipa million 10 kila mwaka. Miaka mi4 ni milion 40. Ila akimaliza chuo mzazi hawezi mpa hta m5 kma mtaji.
Kama michango ya harusi tu.
 
Kama michango ya harusi tu.
Nimekata rasmi kuchangia harusi,

Nilikuwa napata kadi zaidi ya tano kwa mwaka,

Nilikuwa najitahidi sana kuchangia,

Ila mwaka huu only 2 watakaowahi hao hao
 
Mimi nilikua napenda sana tennis..ila nilichezea kichapo siku moja baada yakutoroka shule kwenda kucheza tennis,,,ningeendelea i hope leo ningekua world top seed kibasa



Roger angenitambua vizuri
 
Mruhusu mtoto afuate anachokitaka upate wakina Chid Benz na Amber Lulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…