jimmyfoxxgongo
JF-Expert Member
- Jan 23, 2013
- 5,352
- 9,329
Wakuu amani ya bwana iwe nanyi,
Kwanza kabisa hakuna mzazi hata mmoja ambaye anapenda mwanae au kijana wake asifanikiwe lakini kwa namna moja ama nyingine wazazi wamekuwa ni chanzo cha vijana na watoto wao kutokufanikiwa kwa maana ya kutimiza ndoto zao katika maisha,
Naamini sio mara moja au mbili umekutana na migogoro katika familia kwa sababu tu mtoto hataki kufanya kile wazazi wanachokitaka mfano wazazi wanataka mtoto asome masomo ya sayansi mtoto yeye anataka asome kitu kingine,
Mtoto anataka ajiajiri na sio kuajiriwa lakini hiyo inakuwa ni kesi nyumbani basi ndugu wataitana vikao na vikao wazazi hawataki kuelewa kuwa kijana wao ana maono ambayo huenda yakamfanya kuwa bora zaidi,
Kibaya zaidi huenda ajira yenyewe ndo hizi ikikatwa 60,000/= tu ni majanga,
Wazazi waacheni watoto wawe flexible bahati mbaya sana mnataka watoto wenu wafuate misingi ile ile mliyopita ilhali hakuna cha ziada mlichokifanya mpaka leo
Wazazi mpaka leo hamna uhuru wa kiuchumi bado mnafanya kazi maofisini tena kwa kupelekeshwa sometimes na vijana wadogo wanaofanana umri na watoto wenu lakini ninyi mnataka na vizazi vyenu viishi kama ninyi mlivyoishinkwa stress hata mkiombwa hela ya ada tu ya kawaida majanga
Wazazi waacheni watoto watimize ndoto zao wapeni full support ya watieni moyo
Nawasilisha