Ukiona mwenzako kanyolewa zako tia maji,Wanetu tufanyeje mana kulaumu haijengi na wengi umri mdogo,na inakatisha tamaa kwa wanaondelea,wazazi tufanyeje ili waliopo mashuleni waepuke tatizo,na walio na tatizo tuwasaidieje wanetu waliojijeruhi na kujeruhiwa
Badala ya kutafuta namna ya kuwasaidia hawa vijana na watoto wetu waliofanya vibaya kwenye mitihani yao, Wazazi na wote wanaoitakia mema nchi hii tunapaswa kuinua vichwa na kupaza sauti zetu, tena ikibidi kwa kufanya maandamano makubwa ya kushinikiza kujiuzuru kwa waziri na watendaje wakuu wote katika sekta ya elimu.
Lakini pia tuishinikize serikali ya KIKWETE ifanye mabadiliko makubwa ya kuiboresha sekta ya elimu nchini, kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia, uwepo wa vitendea kazi, mazingira bora ya kuishi walimu, kuboresha maslahi ya walimu.
Tuishinikize serikali ihakikishe ya kuwa wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ni wale tu waliofanya vizuri (NAPENDEKEZA WALIOPATA DIV 1 NA 2).
Pia tuishinikize serikali kusimamisha utoaji wa elimu kwenye shule zote za kata ambazo zina mapungufu makubwa mpaka pale zitakapoboreshwa.
TUACHE SIASA KWENYE ELIMU.
Ndugu zangu na wazazi wenzangu hatuwezi kuendelea kukaa kimya ilhali kwa makusudi mazima serikali iliyopo madarakani imeamua kutengeneza taifa la wajinga na wapumbavu....NI HATARI KWA UHAI WA TAIFA HILI.
Hatupaswi tena kuendelea kukaa kimya ilhali wanazidi kuangamiza taifa hili, wanazidi kutufanya masikini kila uchao.
Fikiria kwa mzazi wa kijijini aliyejibana kila kona ili ampeleke mtoto wake akapate elimu, ametupa pesa kwenye ada, sare, madawati, michango ya ujenzi , ulinzi, mitihani kwa miaka minne, leo mtoto anaambulia sufuri! INAUMA SANA.
TUAMKE WATANZANIA HAWA WALIO MADARAKANI WANATUANGAMIZA, TUCHUKUE HATUA SASA!