Wazazi tuwe na hekima katika haya

Wazazi tuwe na hekima katika haya

Apollo one spaceship

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2021
Posts
245
Reaction score
457
*Mtoto wako anakosea halafu mzazi unapanick unaanza kumkumbushia gharama zote ulizotumia kumsomesha.Umesahau kwamba kusomesha mtoto ni sharti kisheria.Mtoto hakulazimishi,bali sheria ndo inakufunga usomeshe hata kama Ni kwa gharama yoyote ile, kikubwa mtoto apate elimu bora.Wewe heshimu tu sheria, somesha mtoto apate haki yake halafu ukae utulie; hata kama akikataa shule,umeshatimiza wajibu wako.

*Mtoto anakuomba hela ya matumizi shuleni unaanza kumhoji mara "hoo!! hela ya nini??,kwani hamupikiwi shule??."kula chakula cha shule si tumelipia ada".Wengi wa hawa wazazi hawajui au wanajifanya kusahau maisha ya kule shule ya "uji usio na sukari,Ugali na maharage yaliyoungulia na yenye wadudu".Kuna baadhi ya wazazi wanaamini ukimtumia hela mtoto wa kiume eti atahonga wanawake.Ndugu mzazi utamuharibu hata mtoto mwema kwa sababu ataanza udanganyifu ili umtumie hela.Hapo ndo utaongea na walimu fake,utasikia vitu kama 'baba nimevunja plasmodium ya shule'.Kiujumula utaanza kutapeliwa kijanja.Kama hela unayo bora umtumie kwa sababu Ni Haki ya mtoto kuhudumiwa na mzazi wake haswa kwenye mazingira magumu ya hizi shule zetu.

*Kisa eti ni mtoto wako ndo unajijengea imani kwamba fulani ni mtoto wangu tu hana akili ya kujipangia maisha,unaminya uhuru wake hata akikupa wazo unalipinga,unaona akitoa wazo utaonekana mjinga.Hata akiwa chuo labda mwaka wa Kwanza bado unambana tu,huna imani naye hata kwenye shughuli zako unaamini mtoto Ni mtoto hawezi kujijenga mwenyewe.Ndugu waafrika hapa ndo tunapofeli,kila mtu amezaliwa na maono yake kwenye maisha.Tuwape uhuru watoto ila kwa kuwashauri.Anavyoyaona maisha inawezekana huoni kama yeye.

#Tuwape imani watoto kwa sababu inawaongezea kujiamini,tuwape uhuru wa kujieleza;Pia tuwalinde watoto wetu haswa wa kike ambao bila hela yako basi ujue watapata wazazi wazuri wa mitaani ambao watawapa hela,magonjwa na mimba#
 
Bandiko zuri sana limenigusa haswwaa good job
 
Je una watoto?
Kama jibu ni ndio je wana umri gani?
Wamesoma wakafikia viwango gani vya elimu?
Je wanajitegemea?
Umri wako kama hutojali!
 
wakikunyima tafuta mwenyewe uwaprove wrong
 
Kua uyaone! kumbe nilidhani unaongelea uzoefu! Ukija kuwa na watoto ambao watakuwa wamefikia umri wa hao unaowaongelea uje usome hii thread yako ujipime je utakuwa katika mtazamo huo huo?
Sawa ila wazazi wanatakiwa kufahamu nyakati zinabadilika.Wabuni njia za kulea watoto kulingana na muda uliopo kwa sababu changamoto za leo Ni tofauti na zile za miaka ya nyuma.Baadhi wamerithi malezi ya enzi za ujamaa ndo wanalazimisha yatumike mpaka katika kizazi cha leo kitu ambacho hakiwezekani
 
Back
Top Bottom