Ifike wakati Sasa hata hii misaada tunayopewa.... Tuwa tuna-evaluate.... Ni kitu kinachokuwa na manufaa endelevu kwa jamii zetu au ni kitu cha siku moja .... Kesho yake unakwenda haja na habari imeishia hapo.Kaka wamekula siku moja wameenda toilet kesho nani atawapa tena nyama ya mbuzi? Ungekua ni msaada endelevu hata kwa miaka5 sawa.
Ukuta unakaa miaka mia kaka,hao wazazi wanawaza mbali
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hapo hawajalazimishwa tu hali hii sasa wangelazimishwa hali si ingekuwa mbaya zaidi?Halafu kitu kingine.... Tokea lini tukaanza kulazimishana kupokea sadaka/ misaada??
Kama walengwa wamekataa.... What's the logic ya kuanza kulazimishana kupokea sadaka za nyama ya mbuzi na ngombe🤣😂
Muhimu hapo ni kutafuta cha kwako tu na sio kuanza kupanga usaidiwe nini itakuwa vichekesho.Ifike wakati Sasa hata hii misaada tunayopewa.... Tuwa tuna-evaluate.... Ni kitu kinachokuwa na manufaa endelevu kwa jamii zetu au ni kitu cha siku moja .... Kesho yake unakwenda haja na habari imeishia hapo.
Hapa nazungumzia kwenye scenario za misaada inayotolewa kwenye jamii. Hii huwa ipo na itaendelea kuwepo.Muhimu hapo ni kutafuta cha kwako tu na sio kuanza kupanga usaidiwe nini itakuwa vichekesho.
Lakini sio lazima kukubali hiyo sadaka pia ,, nadhani Kama kweli wanalengo la kutoa sadaka Basi walau wange wajengea visima vya maji , Who knows kuhusu usalama wa hizo nyama na usalama wa Afya za hao watakao pewa !?Kama ni sadaka mbona ni nzuri tu kwanini wakatae
Wazazi vilazaWazazi katika shule ya msingi Baraa iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha, wamekataa sadaka ya kuchinja, Mbuzi, Kondoo na Ng'ombe zipatazo 135 zilizotolewa msaada Kwa ajili ya kitoweo cha nyama Kwa wanafunzi wa shule hiyo, wakidai msaada huo unalenga kuwatoa kafara watoto wao.
Msaada huo ambao ulikuwa utolewe tangu Ijumaa ya wiki iliyopita na taasisi ya dini ya kiislamu ya Khair Elkhaleej company LTD ya nchini Misri, ulizua taharuki Katika shule hiyo baada ya wazazi hao kushuhudia Lori lililokuwa limebeba Mbuzi, Kondoo, Ng'ombe na magunia ya mchele Kwa ajili ya kuwapikia chakula wanafunzi hao.
Wakiongea katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Said Mtanda, katika shule hiyo baadhi ya wazazi hao, Monica Meja, Ibrahim Mollel na Godface Godwin walimweleza mkuu huyo wa wilaya ya kwamba hawahitaji msaada huo kwani wamekuwa na hofu juu ya msaada huo kuwa watoto wao kudhulika.
"Sisi wazazi tumekuwa na wasiwasi baada ya kuambiwa kuwa kuna mifugo inakuja kuchinjwa hapa shuleni Kwa ajili ya kitoweo kwa wanafunzi, jambo hili tulipaswa tujulishwe mapema maana hatuna uhakika wa afya za watoto wetu "alisema Monica Meja.
Naye Mzazi mwingine, Godface Godwin alisema suala la kiimani linahitahi ufafanuzi mkubwa Kwa sababu wanaotoa msaada wanaimani yao na sisi hapa tunaimani yetu ndio maana tunahofu na msaada wao ukizingatia kwamba wanyama watakaochinjwa watahitaji kuombewa.
Naye Ibrahim Mollel ambaye ni Mzazi na mwananchi wa kata ya Baraa aliitaka. Taasisi hiyo kuubadilisha msaada huo badala.ya kutoa sadaka ya nyama badala yake wajenge ukuta kuzunguka shule hiyo.
"Mheshimiwa mkuu wa wilaya sisi kama wazazi tumekuwa na hofu juu ya msaada huo wa nyama Kwa watoto wetu unaotokewa na wahisani, tunawaomba wakabadilisha hii sadaka watujengee uzio katika shule yetu,wauze hiyo mifugo Kwa sababu watoto wetu wakija kula wakazulika itakuwa shida sana''alisema
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Said Mtanda aliwatoa hofu wananchi hao Kwa kuwaeleza kwamba wasiwe na wasiwasi Kwa sababu amejiridhisha pasipo shaka kwamba msaada huo ni salama na hauna hofu na maisha ya watu.
Mtanda aliwasihi wananchi hao kupokea msaada huo hao shuleni kwa ajili ya chakula Cha watoto wao kwani ameelekeza mifugo hiyo ichinjwe katika machinjio ya halmashauri na serikali ndio itagawa hizo nyama katika shule zilizoelekezwa za jiji la Arusha.
"Kwa sababu mmekuwa na mashala na msaada huu, mimi sijaja hapa kuwalazimisha mpokee Ila kama hamtaki basi, utaelekezwa Kwa wengine wenye uhitaji Ila suala la kuchangia chakula shuleni ni lazima "alisema Mtanda.
Aidha aliongeza Kwa kutoa maelekezo Kwa wazazi wasiotaka kuchangia wakamatwe na kufikishwa kituo Cha polisi.
Mwakilishi wa Taasisi ya Khair Elkhaleej company LTD hapa nchini ,Jamar Waziri alisema taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa msaada katika nchi mbalimbali kupitia mashule.
Alisema taratibu zao ni kununua mifugo na kuitoka sadaka ya nyama kwenye shule mbalimbali na katika shule za jiji la Arusha walipanga kuchinja mbuzi na Kondoo zipatazo135 ,Ng'ombe, mchele kilo 400,mafuta na Kuni Kwa wanafunzi zaidi ya 2000 katika shule ya Baraa
"Wananchi wamekuwa na hofu wakifikiria watoto wao wanakuja kutolewa kafara na baadhi ya wazazi wakajikuta wakizuia watoto wao wasije shuleni "alisema
Alifafanua kwamba taasisi yao makao yake makuu yapi Egpty nchini Misri na imekuwa ikijohusisha kutoa misaada katika matawi yake ikiwemo Nchi ya Tanzania na Malawi.
Naye Diwani wa kata ya Baraa, Jacob Mollel alisema kuwa msaada huo ulifika katika Kata yake ijumaa iliyopita lakini aliamuru kusitishwa baada ya wazazi kuibuka mashala na msaada huo.
Akiongea katika kikao hicho Leo alisema baadhi ya wazazi wameelimishwa na kukubali kupokea msaada huo laikini baadhi yao bado wanamashaka jambo ambalo aliwasihi wazazi hao kuondoa shaka juu ya wahisani hao kwani wamekubali pia kusaidia katika nyanja mbalimbali za maendeleo katika shule hiyo.
Ends.....
Msaada au sadaka ya kula siku moja ndio muusifie hiviIkumbukwe kuwa Wazungu wa Marekani pia wameshatoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya lishe mashuleni.
Hapo napo watazuka watu wa kudai hao ni Freemasons, wengine watasema hivyo vyakula vinaharibu akili za watoto!
Wakiambiwa kuchanga watoto wao wale wanasema eti, 'walimu watakula' hatuwezi kuchanga!
Watoto wanakaa na njaa kutwa mzima. Wakifeli walimu hawafanyi kazi!
Afrika is shit hole!
Ndio hivyo maana utakuta unapewa msaada wa pesa halafu unaambiwa uitumiaje hiyo pesa yani anakupangia matumizi, bora ule msaada ambao anaulizwa kabisa uchague mwenyewe sasa ukitaka ujengewe uwanja wa mpira au msikiti hapo ni vipaumbele vyako mwenyewe.Hapa nazungumzia kwenye scenario za misaada inayotolewa kwenye jamii. Hii huwa ipo na itaendelea kuwepo.
Ni huyo huyo ALAALA ndio nini?
Mkuu mbona waarabu wanajenga hadi visima vya maji na mambo kibao tu sasa hii sadaka ya nyama ndio iwe shida? Hawajalazimishwa kwa sababu sadaka haulazimishwi ni hiari yako uchukue au ukatae.Msaada au sadaka ya kula siku moja ndio muusifie hivi
Shida sio nyama tuwaelewe vizuri wazazi.. ok wale leo nyama na kesho je?
Kama ni msaada kama mnavyodai basi wangezipa shule hizo mifugo wafuge watoto wanywe maziwa watapata samadi kuweka kwenye bustani za mboga au shamba la mahindi Kwa ufupi shule zitakuwa na miradi ya kujikimu.
Sasa mnashabikia eti wanakataa nyama
Ndiyo wengine wana imani zao kwa nini kudharau imani zao
Kama ni kafara je? Sadaka za kuchinja Kwa nini hawachinji kwao?
Ni upuuzi kukubali kulishwa nyama siku moja eti sadaka
Msaada wa mzungu haufanani na msaada wa mwarabu tuache unafiki
Mzungu atajenga shule hospitali vituo vya kulelea watoto
Kula nyama uingize protini mkuu halafu usizarau kuna wengine nyama hawali makwao ni kama anasa, kuna wengine maji ya kunywa ya baridi tu dili ila kwa wengine ni kitu cha kawaida, hata hivyo watu walielimishwa na wengine wakachukua nyama wameenda kujenga shavu na ukuta watajengewa pia.Kuna punguani hawana akili kabisa. Unanipa msaada ninakataa, kinachofanya upige yowe na kulazimisha niupokee ni nini?
Nini mantiki ya kula nyama siku moja au mbili. Hiyo ni chanjo dhidi ya njaa au ina maajabu gani mpaka mshupaze shingo kulazimisha watu wale
Mkuu hakuna kitu kibaya kama kukosa akili au upumbavu... Nimesikiliza kipindi cha Leo tena clouds media mpaka nikashika kichwa jinsi baadhi ya jamii zetu ilivyojaa ujinga...Ikumbukwe kuwa Wazungu wa Marekani pia wameshatoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya lishe mashuleni.
Hapo napo watazuka watu wa kudai hao ni Freemasons, wengine watasema hivyo vyakula vinaharibu akili za watoto!
Wakiambiwa kuchanga watoto wao wale wanasema eti, 'walimu watakula' hatuwezi kuchanga!
Watoto wanakaa na njaa kutwa mzima. Wakifeli walimu hawafanyi kazi!
Afrika is shit hole!
Ni huyo huyo ALA
Hawa jamaa wao wamekijika kwenye kuinua ubora wa elimu mashuleni na moja ya program zao ni kusaidia chakula mashuleni kwa sababu wamebaini ni tatizo kubwa kwa wanafunzi kukaa shuleni tokea saa moja asubuhi mpaka saa kumi bila kula... So hawawezi kwenda kwenye Magereza coz it's not targeted people..Ni sahihi kabisa. Huo msaada upelekwe huko magerezani na kwenye vituo vya watoto yatima.
Nyama ya siku moja inaongeza shavu? Hii nchi umaskini umezidi kipimo, yani mtu serious karne ya 21 nchi ina miaka 60 imepata uhuru analilia nyama za siku moja aongeze shavu.Kula nyama uingize protini mkuu halafu usizarau kuna wengine nyama hawali makwao ni kama anasa, kuna wengine maji ya kunywa ya baridi tu dili ila kwa wengine ni kitu cha kawaida, hata hivyo watu walielimishwa na wengine wakachukua nyama wameenda kujenga shavu na ukuta watajengewa pia.