Nimekuwa na mahusiano na huyu binti kwa miaka 2 sasa nafsi yangu imeridhika naye na tulipanga baada ya yeye kumaliza masomo tuanze mipango ya ndoa, sasa kamaliza masomo yake....aliwaeleza wazazi wake kuhusu mimi na kwamba tunaitaji kupeleka posa kabla ya mipango mingine ya harusi cha kushangaza baba yake aligoma kwamba binti yake ni mdogo (22yrs) kiukweli sina amani coz tunaishi mikoa tofauti na hata kuonana inakuwa kazi sasa kwa sababu yuko home kwao ni ngumu sana kutoka naona kama naweza mkosa kama hali hii ikiendelea kwa muda mrefu. Yeye yuko tayari na ameridhia tatizo ni mzazi wake na ndiye anapaswa kumsikiliza, imefikia hatua nafikiria kumpa mimba ila kwa upande mwingine naona si sahihi. Naomba msaada wenu wa kimawazo kwa sababu hili swala linaitaji ridhaa ya wazazi ili kujenga uhusiano bora na familia yao