Wazazi walaumiwe na serikali ilaumiwe watoto wadogo wanashinda stendi kufanya biashara

Wazazi walaumiwe na serikali ilaumiwe watoto wadogo wanashinda stendi kufanya biashara

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2023
Posts
418
Reaction score
526
Inapofika msimu wa kuandikisha watoto serikali inazisitiza wakaandikishwe,lakini wakishaanza shule ufuatiliaji wake unapunguwa hali inayopelekea watoto kuzurula mtaani.Wazazi walaumiwe na serikali ilaumiwe watoto wadogo wanashinda stendi kufanya biashara ni aibu tunatengeneza taifa gani?Tazama picha hiyo.

IMG_20240521_103542.jpg
 
Usikute wanaishi na bibi, wazazi walifariki, bibi mlemavu yupo kwenye 90s, hana kipato zaidi ya shamba ambalo akilima ndio anawatuma hao madogo wakauze.
 
Muhimu wajue kusoma na kuandika
Bora yao wanaanza biashara wakiwa wadogo, wanachukua ujuzi wa kutosha
Kuliko waliopo darasani kukariri notes wanamaliza shule na 20's ajira hamna mitaji holaaa..!
 
Aende shule usiku alale njaa, au aende sokoni usiku apate rizki?
Soko nalo ni shule, linatoa somo, na ujuzi pia...
Tulio uza malboro/mifuko ya rambo kipindi tukiwa wadogo mikono juu
 
Tunaharibu hatma ya taifa letu.Nadhani ungetengenezwa ufuatiliaji na usimamizi mzuri wa kuwabaini watoto wasiyoenda shule kutokana na maisha duni halafu kuwaweka mahala pamoja wapate malezi na elimu.Hii ingepunguza uzurulaji na wajinga ktk Taifa.Serikali idhamiriye na kujipanga ktk hili.
 
Back
Top Bottom