Wazazi, walezi mnaonaje hili suala la kufanya kila mtu kuonekana ni ndugu kwa watoto wenu?

Wazazi, walezi mnaonaje hili suala la kufanya kila mtu kuonekana ni ndugu kwa watoto wenu?

mathsjery

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Posts
2,249
Reaction score
1,813
Kuna tabia ya wazazi ama walezi wenye marafiki mbalimbali pia hata majirani kuwaambia watoto wao kuwa, waitane kaka na dada ama mjomba ama aunt. Hapa sijaeleweka ngoja nitoe mfano.

Wewe una mtoto mdogo na jirani yako naye ana mtoto mdogo, yule mtoto wako ukamsikia anamsalimia yule jirani yako shikamoo, basi ukamkemea huku ukisema sema shikamoo mama mdogo ama shikamoo mjomba, ama shikamo bibi.

Huyu mtoto akikuwa akajua kuwa wale si ndugu zake bado ataendelea kuwapa salamu za undugu.

Sasa shida iko hapa:

Je, mwanao akimpenda binti wa rafiki yako wa karibu, ama jirani yako ambaye umekuwa ulimwambia amwite mama mdogo, shangazi au dada je, itakuwa rahisi kwake kumuoa/kuolewa naye maana bado kuna hiyo mentality ndani yake ya kuitana kaka na dada sijui mjomba na hakuna undugu wowote.

Vipi hamna namna ya kumsalimu mtu mzima asiye ndugu yako? Hivi ndo tunakosa wake zetu kwa undugu fake.

NB maoni yenu
 
Kwani shida ikwapi
Mfano unataka kuoa binti wa mtu unayemwita shangazi au mama mdogo, tena shangazi huyo au mama mdogo wamezoeana kama ndugu na wazazi wako kuna hali flani hivi, mfano mimi naitwa mjomba na mtu ambaye labda ningetaka kumwoa kisa baba yangu aliitwa baba na jirani yangu hadi mzee huwatania wajukuu wake(with no blood sharing). Inakuaje.
 
Ni unafiki tu, hebu mpe mimba huyo binti alafu tuone itakuaje
 
Back
Top Bottom