Mgombezi
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 610
- 181
Wapendwa, nimepokea ujumbe huu kutoka kwa rafiki yangu akiniomba ushauri; nimeamua kuleta hapa kisa hiki nikiwa na imani ya kupokea mawazo mazuri.
Nimekua katika mahusiano na watu tofauti ila mvulana wangu wa kwanza ndo mpaka nyumban walikua wanamjua, hatukua katka mahusiano kwa miaka 8 na hatujawasiliana kwa miaka 3, juz narud nyumban likizo nakuta ameleta posa nyumban na wazaz wamepokea nilipofika wameniambia nilikataa wao kupokea hiyo posa bila kunishirikisha kwan tayar nina mtu wangu ambaye nina mpenda na tuko nae katka mahusiano, kiukwel hivi karibun mpz wang huyu pia alikua ana mpango wa kuja nyumban kujtambulisha na kufanya mchakato wa kuanza maandalizi ya posa na mahali, ila wazaz na ndug wooote walinikalisha chin na kunisema sana kuwa wenyewe wanamjua huyo mtu wang wa kwanza hawamtambui huyu niliye nae, mipango imefanyika mpaka mahali imetolewa juz na engagement ring nimevalishwa ingawa sijaridhia kwa moyo wang, naomba ushaur wako, hivi mahali ikitolewa inaweza kurudishwa? nini hupelekea mahal kurudishwa? nahitaj kujua maana sitak kumuumiza mpz wang nliyenae kwan mpaka saa hii yuko vibaya na hoi, naomba nisaidie.