MSHINO
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,069
- 713
Ndugu wana jamii, mimi ni mtanzania mwenzenu naomba msaada kujua kama wazazi wa marahemu wanaweza kupata mgao wa mirathi baada ya mtoto wao kufariki; naomba nitoe ufafanuzi km ifuatavyo.
kuna wazee ambao ni wakwe zangu na ni wazee sana km miaka 75-85. walifanikiwa kupata watoto 4 wa kike na 1 wa kiume. watoto wa kike wote wameolewa bahati mbaya mtoto wa kiume ambaye alikuwa anawasaidia wazee hawa alifariki miaka 10 iliyopita kwa ajari. katika uhai wake alikuwa na rasilimali mojawapo ni nyumba moja mkoani na nyingine mbili Dar es salaam, marehemu aliwahi kuoa mke wa kwanza na wakachana akamacha na watoto 3, 2 wa kiume na 1 wa kike. lakina katika pita pita alizaa watoto wengine 3 kwa akina mama wawili tofauti watoto watoto wote ni wa kike. baada ya kuachana na mke wa kwanza alioa mke mwengine ambaye walifanikiwa kupata watoto wa 3, mmoja wa kike na wawili wa kiume, na kufanikiwa kujenga nyumba zote 3 moja (1) mkoani na 2 Dar. baada ya kifo cha marehemu familia ilikaa kwa pamoja na kuamua km ifuatavyo.
1. Mke wa marehemu awe msimamizi wa Mirathi.
2. mali zilizopo Dar ziwe urithi wa watoto wa Dar es salaam.
3. Mali za mkoani ziwe mali za watoto wa mkoani.
4. Wazazi wapewe chumba kimoja cha biashara kwenye nyumba ya Dar ili kodi itakayokuwa inapatikana iwasiadie.
Makubaliano haya yalisimamiwa na babu wa wajukuu yaani baba wa marehemu na makubaliano hayo yalipelekwa mahakamani yawe kisheria.
Baada ya mzee kurudi mkoani aliwaita wajukuu zake na kuwakabidhi kiwanja amacho walikiuza na kujenga sehemu nyingine. nyumba ya mkoani iliapangishwa kwa kiasi cha shilingi 30,000/= kwa mwezi na hivyo kuwasaidia wazee kupunguza ugumu wa maisha. baada ya miaka hiyo watoto wa mkoani wameomba wakabidhiwe nyumba wauze ili wagawane pesa, babu amakubari lkn mahakama ikakataa mpaka msimamizi wa mirathi afike, lkn msimamizi wa mirathi yuko Dar (yaani mke wa marehemu) msimamizi alimwomba hakimu kuwa babu asaini kwa niaba ili watoto wakabidhiwe nyumba. Babu aliomba kuwa na wao km wazazi na hawana msaidizi wapewe pesa kidogo na watoto walikubari kutoa laki tano babu akaweka saini (dole gumba). lkn baada ya kuweka saini hakimu alimwambia kuwa watoto wataamua wampe au wasimpe kwaani haiwahusu wazazi ni mali ya watoto. Nyumba itauzwa kwa milioni 50. Wazee wanaona km wajukuu hawajawatendea haki kuwanyima pesa wakati hawajiwezi.
Je wazee wana haki hapa? imani ya familia ni waisalmu.
Aksanteni naombeni msaada.