Wazazi wasiojiweza wana haki kupata mgao?

MSHINO

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,069
Reaction score
713
Ndugu wana jamii, mimi ni mtanzania mwenzenu naomba msaada kujua kama wazazi wa marahemu wanaweza kupata mgao wa mirathi baada ya mtoto wao kufariki; naomba nitoe ufafanuzi km ifuatavyo.

kuna wazee ambao ni wakwe zangu na ni wazee sana km miaka 75-85. walifanikiwa kupata watoto 4 wa kike na 1 wa kiume. watoto wa kike wote wameolewa bahati mbaya mtoto wa kiume ambaye alikuwa anawasaidia wazee hawa alifariki miaka 10 iliyopita kwa ajari. katika uhai wake alikuwa na rasilimali mojawapo ni nyumba moja mkoani na nyingine mbili Dar es salaam, marehemu aliwahi kuoa mke wa kwanza na wakachana akamacha na watoto 3, 2 wa kiume na 1 wa kike. lakina katika pita pita alizaa watoto wengine 3 kwa akina mama wawili tofauti watoto watoto wote ni wa kike. baada ya kuachana na mke wa kwanza alioa mke mwengine ambaye walifanikiwa kupata watoto wa 3, mmoja wa kike na wawili wa kiume, na kufanikiwa kujenga nyumba zote 3 moja (1) mkoani na 2 Dar. baada ya kifo cha marehemu familia ilikaa kwa pamoja na kuamua km ifuatavyo.
1. Mke wa marehemu awe msimamizi wa Mirathi.
2. mali zilizopo Dar ziwe urithi wa watoto wa Dar es salaam.
3. Mali za mkoani ziwe mali za watoto wa mkoani.
4. Wazazi wapewe chumba kimoja cha biashara kwenye nyumba ya Dar ili kodi itakayokuwa inapatikana iwasiadie.

Makubaliano haya yalisimamiwa na babu wa wajukuu yaani baba wa marehemu na makubaliano hayo yalipelekwa mahakamani yawe kisheria.

Baada ya mzee kurudi mkoani aliwaita wajukuu zake na kuwakabidhi kiwanja amacho walikiuza na kujenga sehemu nyingine. nyumba ya mkoani iliapangishwa kwa kiasi cha shilingi 30,000/= kwa mwezi na hivyo kuwasaidia wazee kupunguza ugumu wa maisha. baada ya miaka hiyo watoto wa mkoani wameomba wakabidhiwe nyumba wauze ili wagawane pesa, babu amakubari lkn mahakama ikakataa mpaka msimamizi wa mirathi afike, lkn msimamizi wa mirathi yuko Dar (yaani mke wa marehemu) msimamizi alimwomba hakimu kuwa babu asaini kwa niaba ili watoto wakabidhiwe nyumba. Babu aliomba kuwa na wao km wazazi na hawana msaidizi wapewe pesa kidogo na watoto walikubari kutoa laki tano babu akaweka saini (dole gumba). lkn baada ya kuweka saini hakimu alimwambia kuwa watoto wataamua wampe au wasimpe kwaani haiwahusu wazazi ni mali ya watoto. Nyumba itauzwa kwa milioni 50. Wazee wanaona km wajukuu hawajawatendea haki kuwanyima pesa wakati hawajiwezi.

Je wazee wana haki hapa? imani ya familia ni waisalmu.

Aksanteni naombeni msaada.
 
Kuna makubaliano na sheria.Kuna sheria ya nchi na kiislam.Wachague ipi waitumie.Kama walikubaliana, wawape tu wazee wao, mana hawajiwezi, na wao ndo wakuwasaidia.Kwani wazee hawawezi kuathirika ikiwa wajukuu wapo.Ni mtazamo wangu
 
Kisheria wazazi wa marehemu wana haki ya kupewa urithi wa mtoto wao. Vyovyoye vile iwavo kinachoangaliwa ni zaidi ni maamuzi ya msimamizi wa mirathi.
 
Aksante sana, msimamizi wa mirathi mama wa nyumbani uwezo wake wa kuelewa ni mdogo, yeye binafsi aliwaambia wajukuu wawape babu zao milioni 5 katika mauzo ya milioni 50. wajukuu hawataki na hakimu ndiyo amesimamia kuwa siyo lazima. wazee walitegemea kodi ya nyumba ili kujikimu, watoto waliobaki ni wa kike wameolewa ni mama wa nyumbani msaada mpaka waume zao watoe chochote.
 
Kuna taratibu Zinazoongoza uendeshaji, usimizi na mgawanyo wa mali ya mirathi. Kwa hapa kwetu (TZ) mirathi yeyote huendeshwa au huwa kati ya mafungu matatu ya kisheria ambayo ni:
(1) Sheria za nchi (za serikali)
(2) sheria za kidini (kiislamu au kikristu)
(3) sheria za kimila
Ili kufaham mirathi fulani itaamuliwa kwa sheria ipi si jambo la kupendezwa na sheria moja kati ya hizo bali kwa mujibu wa kifungu cha 88 cha sheria ya usimamizi wa mirathi, inaeleza namna ya kufikia hatua ya kuipata sheria ya kuitumia kati ya hizo.
Niielezee sheria ya kidini hususani ya kiislam ambayo umedai ndiyo imani ya familia.
Kitu kikubwa kitaangaliwa wosia kama umeachwa, kama marehemu kasema mali yake isimamiwe na kugawanywa kiislam ktk wosia sharia ya kiislam itahusika au kama wosia haupo utaangaliwa mwenendo wa marehem mfano: alioa ndoa za kiislam? au alikuwa mswalihina? n.k, kama jibu ni ndiyo sharia ya kiislam itatumika kwenye mirathi yake.
Warithi kwa mujibu wa sharia za kiislam, wameorodheshwa ktk Qur'an na kile watachopata (shares), kila mmoja imeelezwa atapata nini, mfano mke wa marehemu share yake ni;
1/8 ikiwa marehem kaacha mtoto/watoto
1/4 ikiwa marehemu hakuacha mtoto/watoto
NB: kwa mujibu wa sharia za kiislam mtoto/watoto ni wale halali sio wa nje ya ndoa

Kulijibu swali lako kama mirathi ilijikita ktk sharia za kiislam huyo baba ana HAKI ya kupata urithi/ mgao wa hiyo nyumba kwa sababu ni mmoja wa warithi waliotajwa ktk Qur'an
Kwa upande mwingine kosa lilifanyika kugawa mirathi ya marehemu kwa kuangalia matumbo ya mama, yaani nyumba/mali fulani apewe bi mkubwa na wanawe na nyumba/mali fulan apewe mke mwingine au watoto wa mke mwingine, hii si sawa ktk mirathi ya kiislam kwa sababu kila mrithi amepewa hesabu yake ktk Qur'an atachopata siyo kukadiria tu.
Ilitakiwa mali zote za marehemu zikusanywe/zitambuliwe halafu baba, mama mke/wake, watoto wapate kwa mujibu wa shares(mgao) wao kwenye Qur'an.
mfano wa mama wa marehemu
1/6 kama marehem kaacha watoto
1/3 kama marehemu hakuacha mtoto

mpaka hapa natumaini umeongeza kitu
 
Umefafanua vizuri sana.
 
Back
Top Bottom