Habari yenu wandugu...natumaini wote m-wazima wa afya!

Linapokuja swala la mahusiano/ndoa na watoto waliozaliwa kabla hua hatuachi kuongelea mama wa kambo na malezi ya watoto.Naongelea wamama tu maana wababa wengi hua hawana matatizo wawe wazazi kabisa au walezi(wale wa kambo) linapokuja swala la mzazi mwenza kua na mahusiano mapya au wale wa kambo kulea watoto wa mwenzie tofauti na wa mama!

Nwy mara nyingi wasiwasi hua unakua kwa watoto zaidi na malezi/uwepo wa mama wa kambo.Tunasahau kwamba hata yule mwanamke mpya anaweza akanyanyasika na uwepo wa watoto wasio wake pamoja na mama yao bila kusahau ndoa yake kuyumbishwa kama mti usio na nguvu dhidi ya upepo.Kama tunavyojua wakati mwingine au niseme baadhi ya wanawake hua na vinyongo..gubu..chuki kwa wazazi wenzao kwa kuachana nao...na kitendo cha mwanaume kupata mwanamke mwingine na kuoa hakiwi cha furaha kwa wote!Sasa wanawake wa aina hii wanaweza kutumia watoto wao kuyumbisha ndoa ya wengine pia kusambaza chuki.Ila muhimu hapa ni hili la kuyumbisha ndoa...kuharibu au hata kuondoa kabisa amani ndani ya nyumba ya mwanamke mwingine kwa kutengeneza mazingira ya kuwachanganya wapendanao!Unakuta mwenye watoto anawatumia wanae kumuendesha mwanaume kama gari moshi kitu ambacho hakiwezi kumfurahisha mwenye mume.Yani kama aliyeolewa ni mwepesi wa kukasirika na kubugidhiwa ndoa inaweza ikaishia kuzimu.

Nakumbuka kuna mtu wangu wa karibu alipata shida sana kipindi cha mwanzo cha ndoa yake.Mwenye watoto alikua ni mkorofi sana na kila anachofanya anafanya kukomoa tu.Watoto amewahamishia shule ya kawaida ila ada anapokea ya shule ya international.Anawadanganya watoto wakubali kwamba wanaumwa ili amchune baba wa watu mpaka abaki mifupa tu.Ilikua kazi kweli maana unakuta mke alishataka/hitaji kitu akaambiwa pesa hamna bwana mwezi huu tufanye kitu flani alafu mwezi ujao tutafanya utakavyo...alafu mwenzie anapiga na kuagiza wala sio anaomba awe amepata maelfu kadhaa ndani ya masaa na anapata bila ubishi. Alilia mpaka baadae alipogundua kwamba sio kosa la mume wake...yeye tatizo lake ni mapenzi kwa wanawe na woga kwa yule mama.Ikabidi aanze kumshauri mumewe asiwe mwepesi wa kukubali kuchezewa na yule mama ndo mume nae akawa mgumu na kukataa kusukumwa kama mkokoteni!

Kwahiyo naomba niwaulize wababa wenye mtoto/watoto tayari..hawapo kwenye ndoa ila wanatarajia kuwa siku moja...mmejiandaa vipi kukabiliana na changamoto zitakazosababishwa na juhudi za wazazi wenza kutaka kuvuruga ndo zenu na kuwaondolea amani ndani ya nyumba????!

Binafsi naamini mwanaume akikataa kuchezewa na mzazi mwenza basi haitatokea...hivyo basi nawashauri muwe mnawapa wale mlio nao kipaumbele.Kama akiashiria kua kuna matatizo yanayosababishwa na mzazi mwenzio hakikisha tu haitokani na chuki kisha yafanyie kazi.Usikubali kuharibiwa ndoa/mahusiano yako kwa kisingizio cha watoto ambao hata hawahusiki.Usikubali kutumiwa wala kuchezewa....mahitaji mengine ya mtoto nunua mwenyewe usije ukageuzwa kitega uchumi.Kwa wamama ukijikuta kwenye situation kama hii jitahidi kua mvumilivu na mshauri wa mwenzio...pia jitahidi matatizo yatakayosababishwa na mama mtu yasizae chuki kwa mtoto!!

Usiku mwema kwa mnaojiandaa kulala...jioni njema kwa mnaomalizia malizia siku na siku njema mnaoianza!Poleni kwa thread ndefu!

Lizzy Leo Umenishika Pabaya sana,nahisi Umeziminya korodani zangu,kulia nashindwa kucheka nashindwa,am just on tenterhook knowing not what to do!!
UMENIGUSA!! Mimi nimezaa na Mwanamke mmoja wa Kichaga watoto wawili,wa kwanza nilimzaa nikiwa na Miaka 24 na Wa Pili nikiwa na Miaka 25, I am 29 years old now approaching 30;the first one is 5 yrs old the second is 4 yrs!! Ni hadithi ndefu kidogo lakini kifupi sikuwa nimepanga kuishi na huyu Mwanamke wala kuzaa hawa watoto during then!! I wudnt like to go into details but Sikuwahi kumpenda huyu Mwanamke(Ilikuwa Uhuni wangu tu) na wala simpendi sasa but I LOVE THE KIDS ILE MBAYA,I TAKE CARE OF THEM,I GV THEM MY LOVE,MY TIME AND MY SUPPORT!!
Natazamia kumwezesha huyu Mwanamke kama uwezo utaruhusu kumjengea nyumba na kumpa some small business ili asimame mwenyewe!! Its hard to live with someone u dnt love although sijawahi kum-mistreat!! On the other hand wala sijampata wala kumtafuta mwanamke wa Kumpenda!!
Wasiwasi wangu Mimi sio kusumbuliwa na huyu Mama wa watoto wangu,hilo haliwezekani hata kwa sekunde,naujua uwezo wangu wa kudhibiti hila na Usimamizi!!!
Wasiwasi wangu siku zote umekuwa kama huyo Mama mtarajiwa atawapenda na kuwakubali watoto wangu na nitapenda niishi nao coz wanakamilisha Furaha yangu hapa duniani!!
Nitajitahidi kuwa-influence watoto wampende Mama mtarajiwa na nitaweka mikakati kabisa ya makusudi kabisa kutimiza azma hiyo e.g Nitafanya kadri ionekanavyo ionekane kama Yeye(Mama mpya) ndiyo anaewanunulia zawadi zawadi,mavazi n.k pamoja na kumsifia frm time to time kuhusu jinsi anavyowapenda!!
Kwa upande wa watoto sina shaka,kwa sababu ni watoto wangu najua nitawamudu,TATIZO huyo wa Mama Mtarajiwa,sijajua what i will do in case she shows signs of indifference to them!!
When It comes to my Children,i can go miles to defend them!! Please advise people!!