WAZAZI WETU JAMANI...Wazazi!

WAZAZI WETU JAMANI...Wazazi!

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
3,811
Reaction score
1,607
Hii ni hadithi tu lakini ndni yake kuna ukweli na mafunzo.
Bwana mmoja, kwa kushirikiana na mke wake, walikuwa wanamdhalilisha babake yule bwana. Mfano, wakati wa kula walikuwa, wanampa chakula katika vyombo chakavu, wanamtenga hawakai nae mezani kwa sababu wakati anakula anadondosha, anatoka mate ovyo n.k.

Siku moja wakati wa chakula walikuwa wanamtafuta mtoto wao msichana akawa haonekani. Walimtafuta hatimaye wakamkuta yuko uwani anachezea udongo mfinyanzi.

Wakati wa kula tayari, unafanya nini hapo?", babake alimwuliza.
"Ninatengeneza sahani na vikombe kwa ajili yenu mtakapokuwa wazee kama babu".

Ndugu zangu:
Tusisahau tabu walizopata mama zetu tukiwa tumboni miezi bila kujua kama tutazaliwa hai au tumekufa, wazima au walemavu.

Tusisahau pale tulipokuwa wachanga tulienda haja mwilini mwao.

Tusisahau maili walizokuwa wanatembea usiku chumbani, sisi mikononi, migongoni au mabegani mwao.

Tusisahau tulipokuwa tunalia bila ya wao kujua tuna nini wakati bado hutujui kusema.

Tusisahau walivyokuwa wanajinyima hali na mali ili kutupa malezi, hifadhi, ulinzi, chakula, nguo, matibabu, elimu....

Na zaidi, tusisahau kuwa chochote tunachomiliki, hadhi yoyte tulonayo, wasingekuwa wao tusingefika hapa tulipo leo.

Tukumbuke, tunavyowafanyia wazazi wetu leo, watoto wetu wanaweza kutufanyia hivyohivyo. Tusije wakatutengenezea sahani za udongo tutapokuwa wazee kama babu.
 
Ni kweli kabisa Mammamia...bila wazazi wetu tusingekuwa hapa....na ukitaka uendelee kubarikiwa, waheshimu na watii wazazi wako, hakika siku zako za kuishi hapa duniani zitaongezeka.

Barikiwa kwa hadithi nzuri.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
aisee!!
Tusisahau maisha ni mduara! Unaanza utotoni, ukidonsha udenda, ukijisadia kwenye nguo, ukiwa hujiwezi kwa lolote.Wazazi wangetaka wangeweza hata kukuua! Hawakufanya hivyo.Badala yake wakakulea kwa upendo, wakakulinda, wakajitolea starehe zao wakakupa wewe kila ulichohitaji.Ulipougua wakakesha wakikuuguza.Wakajinyima ili upate elimu iliyokuwezesha kupata kazi nzuri.Mnakumbuka wimbo wa "sweet mother I will never forget you...the suffering you suffered for me"!?

Kumbuka wazazi wanazeeka na kurudia utoto na ni wajibu wetu kuwalea. Watakuwa wagonjwa na wasiojiweza shauri ya uzee.Watadondosha udenda kama ulivyodondosha wewe na kipindi kile waliona raha na ufahari kukufuta na hata ulipowatemea hawakuona kinyaa!

Wewe leo uko kijana, una nguvu , unajidai na sura yako nzuri isiyo na makunyanzi! Unaona aibu kuonekana na wazee wako wenye makunyanzi! Unaona kero na tabu kuwahudumia.Hutaki hata watumie vyombo vyako!!!

What goes round, comes round!!

Tujihadhari sana na tabia hizi, tuwaenzi wazee wetu ili nasi tukijaaliwa tuje kuenziwa.
 
Hii ni hadithi tu lakini ndni yake kuna ukweli na mafunzo.
Bwana mmoja, kwa kushirikiana na mke wake, walikuwa wanamdhalilisha babake yule bwana. Mfano, wakati wa kula walikuwa, wanampa chakula katika vyombo chakavu, wanamtenga hawakai nae mezani kwa sababu wakati anakula anadondosha, anatoka mate ovyo n.k.

Siku moja wakati wa chakula walikuwa wanamtafuta mtoto wao msichana akawa haonekani. Walimtafuta hatimaye wakamkuta yuko uwani anachezea udongo mfinyanzi.

Wakati wa kula tayari, unafanya nini hapo?", babake alimwuliza.
"Ninatengeneza sahani na vikombe kwa ajili yenu mtakapokuwa wazee kama babu".

Ndugu zangu:
Tusisahau tabu walizopata mama zetu tukiwa tumboni miezi bila kujua kama tutazaliwa hai au tumekufa, wazima au walemavu.

Tusisahau pale tulipokuwa wachanga tulienda haja mwilini mwao.

Tusisahau maili walizokuwa wanatembea usiku chumbani, sisi mikononi, migongoni au mabegani mwao.

Tusisahau tulipokuwa tunalia bila ya wao kujua tuna nini wakati bado hutujui kusema.

Tusisahau walivyokuwa wanajinyima hali na mali ili kutupa malezi, hifadhi, ulinzi, chakula, nguo, matibabu, elimu....

Na zaidi, tusisahau kuwa chochote tunachomiliki, hadhi yoyte tulonayo, wasingekuwa wao tusingefika hapa tulipo leo.

Tukumbuke, tunavyowafanyia wazazi wetu leo, watoto wetu wanaweza kutufanyia hivyohivyo. Tusije wakatutengenezea sahani za udongo tutapokuwa wazee kama babu.

Naam Mkuu maneno mazito sana hayo. Siku zote tusisahau kwamba kabla hujafa hujaumbika.

http://www.youtube.com/watch?v=dW5BgMgLuiA
 
Maneno mazito na mazuri. Watoto hutakiwa washindane kuwafanyia mema wazazi wao na si kuwabughudhi na kuwadharau eti kwa kuwa wamezeeka. Jee vijana wa sasa wanaelekea wapi?
 
....ahsante my dear,wazazi ni Mungu wa pili hapa duniani. Tunawapende na kuwaheshimu wazazi wetu.
 
Asante sana mammamia ni ujumbe mzuri sana.
Ni wajibu wetu kuwatunza,kuwathamini,kuwaheshimu wazazi wetu.
Hata mungu ametuambia tuwaheshimu sana wazazi wetu ili
siku zetu za kuishi hapa duniani ziwe nyingi na zenye baraka.
 
Back
Top Bottom