Mpango?????? But hawapewi......bring us facts dude
Mpango means project, hii ni project ya muda mrefu Tanzania
TASAF III YANUFAISHA
KAYA MASKINI 5,268
MANISPAA YA TABORA
Kaya maskini zipatao 5,268 katika halmashauri
ya Manispaa ya Tabora zimewezeshwa na
serikali kiasi cha sh 1,047,340,000 kupitia
Mpango wake wa kunusuru kaya maskini
TASAF awamu ya tatu.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri ya manispaa hiyo Bosco
Ndunguru katika kikao cha baraza la madiwani
kilichoketi juzi katika ukumbi wa manispaa
hiyo.
Amesema jumla ya kaya 8,402 zilitambuliwa
katika mpango huo na kuwasilishwa majina
yao TASAF Makao Makuu ambapo kaya 5,272
zilithibitishwa na mfumo wa kompyuta huku
kaya 3,123 zikikataliwa na mfumo kwa
kutokidhi vigezo vilivyowekwa.
Aliongeza kuwa baada ya mchakato huo kaya
5,268 ziliandikishwa na kuingizwa katika
mfumo wa malipo ila kaya 9 hazikuonekana.
Alifafanua kuwa katika kipindi cha kuanzia
Julai-Agosti 2016 hadi Mei-Juni 2017 jumla ya
fedha zote za mpango huo zilizopokelewa
ikiwemo za usimamizi ni sh 1,243,959,785
huku fedha za walengwa zikiwa kiasi cha sh
1,091,160,000.
Alibainisha kuwa fedha zilizolipwa kwa
walengwa ni kiasi cha sh 1,047,340,000 huku
akitaja fedha zilizobakia na kurejeshwa Makao
Makuu kuwa ni kiasi cha sh 44,264,000.
Ndunguru alisema mpango huo umekuwa na
manufaa mengi sana kwa familia zilizoko
katika kaya hizo maskini kwani kaya hizo
zimeweza kupeleka watoto wao shule tofauti
na awali jambo ambalo limechochea
mahudhurio mazuri ya wanafunzi mashuleni.
Alisema fedha hizo zimewezesha kaya hizo
kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi ili
kujiongezea kipato katika kaya zao, huku
akitaja baadhi ya miradi iliyoanzishwa kuwa ni
ufugaji kuku, mbuzi, ng’ombe na mabanda ya
biashara ndogondogo.
Alisema mpango huo umeweza kunusuru
familia nyingi na kuongeza umri wa kuishi
kutokana na kupata maitaji kama fedha za
kununua vyakula kuliko kama ilivyokuwa hapo
awali.
Alitaja baadhi ya changamoto zinazokwamisha
zoezi hilo kuwa ni pungufu ufu wa fedha za
uwezeshaji ngazi za vijiji, kupunguza ufanisi
wa kamati ya mradi na halmashauri za kijiji za
kufuatilia maendeleo ya
walengwa.
Ndunguru alisisitiza haja ya kuendelea
kuimarishaji vikundi vya ujasiliamali kwa vijana
na wanawake ambapo wilaya inavyo vikundi
vya wanawake 494 na vijana vikundi 184
ikiwa ni jitiada za kutekeleza
agizo la kuvijengea uwezo vikundi hivyo.
Aliongeza kuwa halmashauri imetenga maeneo
3 kwa ajili ya uendelezaji wa viwanda
vidogovidogo vya vijana na uendelezaji wa
miradi ya maendeleo pia uhamasisha
wananchi katika kujenga nyumba bora ikiwa ni
ajenda ya kudumu ambapo mwitikio wa jambo
hilo bado ni mdogo kutokana na kipato.
Aidha aliwakumbusha umuhimu wa kujituma
zaidi katika miradi yao ili waweze kuongeza
kipato chao huku akiwataka kutopoteza fursa
hiyo akasisitiza kila mmoja wasipoteze fursa
hiyo hivyo.
Na Mussa Mbeho, Tabora