Wazee Kenya kupokea ksh 4000 kwa mwezi

Tatizo wa Kenya kiswahili hamjui, wewe ukisikia Mpango unapata maana gani?

Tasaf ni Mpango wa muda mrefu Tanzania umelenga kusaidia familia maskini

Waliotafuna pesa za TASAF, kiama chao chakaribia | East Africa Television
Eti kiswahili hatukijui? Sasa tunaongea kuhusu wazee afu wewe unatuekea ushahidi wa pesa za masikini zilivotafunwa? Au kutafunwa kwa kizaramo ndo inamaanisha nini? Wewe ndo hujui kiswahili. Kenya pia kuna hela wanazowapa vikundi vya kina mama na vijana. Hapa tunaongea kuhusu hela ambazo wanapewa wazee wa 65+. Wamekuwa wakikabidhiwa hela hizi siku nyingi tu lakini sasa imekuwa ni kshs 4,000. Acha kutuzingua na stori ndefu ndefu blah blah nyingi.
 
Macho kuvimba [emoji34] Tutabaki kutingisha visibo vya peni na kengele tu,ninacho kiweza mimi kama mimi ni kufanya usafi JUMA MOSI [emoji57][emoji57]
 
Akili za kitz hizo, kwao mipango yoyote huko tz ni sawa tu na chochote kile ambacho wakenya wanakifanya kweli. Muda usokuwa mfupi utasikia wameanza zile zao za JPM atafanya hayo. Hata mawaziri husika sijasikia hata siku moja wakiwataja kwa jina.
Ninachokiona wakenya hamuelewi kiswahili. Mnajua vizuri maana ya mpango?? When you are paying on plan, unakuwa haulipi?? Au plan kwa kiswahili sio mpango??
 
Kwanza Tanzania wazee wanatibiwa bure kwenye hospitals za serikali na pregnant women wanatibiwa bure hawalipi hata shiling
 
Reactions: Oii
Kwanza Tanzania wazee wanatibiwa bure kwenye hospitals za serikali na pregnant women wanatibiwa bure hawalipi hata shiling
Kipya ni kipi hapo? Acha kutibiwa tu, in Kenya pregnant women give birth free of charge. Wakishazaa, watoto wakifika umri wa kuenda shule wanaingia shule bure, bila karo. Zaidi ya hiyo wanafanyiwa shopping, vitabu bure, sanduku bure, gondoro hadi na blanketi! Mkuu 1academ njoo humu jombaa, uwaeleze tanavofanyaga. πŸ˜€
 
Kipya ni kipi hapo? Acha kutibiwa tu, in Kenya pregnant women give birth free of charge. Wakishazaa, watoto wakifika umri wa kuenda shule wanaingia shule bure, bila karo.
Katika hayo mambo hakuna tofauti,
Wazee
Wajawazito
Kujifungua
Watoto chini ya miaka mitano
Std 1 hadi Form four hivi vyote ni bure, kenya na tz!

Vipo vya kubishana lakini si kwa masuala kama haya.
Japo sijui kama kenya elimu bure mnatoa hadi form 4
 
Kwanza Tanzania wazee wanatibiwa bure kwenye hospitals za serikali na pregnant women wanatibiwa bure hawalipi hata shiling

 

Attachments

Mbona mim bibi yangu hajawah pewa wala sijawah ona
Nahisi hujasoma vizuri hizo links na attachments nilizoweka!

Lakini ngoja nikwambie kwa kifupi!

Sio kuwa wazee wote wako eligible kupewa hizo pesa, ila ni wale maskini ZAIDI. (neno zaidi hapa lina maana kubwa). Hivyo yawezekana bibi yako akawa ni mzee lakini sio MASKINI ZAIDI kwenye eneo analokaa!

Kuhusu kutosikia, hilo ni tatizo lako binafsi. Lakini mpango huu upo mikoa yote ya tanzania (bara na visiwani) wilaya zote na vijiji/mitaa ilivyochaguliwa vilivyoonekana vina umaskini mkubwa kupitia sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Malipo yanatolewa kila mwezi, lakini kwa sababu ya changamoto mbali mbali, walengwa hupokea pesa zao kila baada ya miezi 2, ikiwa ni pesa ya mikupuo ya miezi miwili.

Kwa malipo ya January na February 2018, ulipaji kwa Tanzania nzima unategemewa kufanyika kati ya trh 22 January hadi 2 February 2018.
Sasa kazi kwako, fuatilia wilaya unayoishi ujue mitaa/au vijiji vilivyo kwenye mpango utajua kinachoendelea.
Unaweza kupita hapa kwa msaada zaidi. Welcome to TASAF website

Kila la kheri.
 
Yaan kaka mi, hata sisomi maneno yako,bye naenda zangu chit chat
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Dah, lazima siku moja ntafika huko chit chat pia. Isije ikawa kuna mazuri yananipita wakati nazubaa tu huku Kenya news.
Hehehe karibu,,nyie mmekazana na mavitu magumuu sie hatutaki bana yanatuongezea stress karibu kule no stress
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…