RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara - 35:
Right Marker
Dar es salaam
Unamkuta mtu tangu amezaliwa ameishi maisha magumu, ugumu wa maisha umemtafuna kwa miaka 50. Anaanza kufanikiwa (kushika pesa) akiwa na miaka 51 baada ya kuuza shamba lake la miti. Sasa tazama vituko vyake mjini!
Mnashangaa!! Huyu mzee mbona anafanya mambo ya kitoto mtaani ambayo hayaendani na umri wake? - Kumbe mwenzenu aliruka hatua nyingi za ukuaji hivyo matukio mengi yalimpita kutokana na ugumu wa maisha.
• Alipokuwa na umri wa miaka 18 - 50 hakuwa na hela hivyo mabinti walimkataa, na kwa bahati mbaya hata ule umri wa kucheza KOMBOLELA mabinti walimkwepa hivyo alikuwa akijificha porini na kwenye mapagala pekee yake. Sasahivi amepata hela analipiza hatua aliyoiruka - analala na vibinti vya miaka 18 - 20.
• Alipokuwa na umri wa miaka 18 - 50 hakuweza kunywa pombe za maana kutokana na umasikini. Sasahivi ameshika pesa analipiza hatua aliyoiruka - hivyo anakunywa pombe mpaka anajikojolea.
• Alipokuwa na umri kati ya miaka 18 - 50 hakuweza kumiliki hata pikipiki. Sasahivi amenunua Crown Athlete amefunga mziki mnene utafikiri Fiesta ya Wasafi Festival. Jioni anakwenda kupark gari kwenye viunga vya Chuo anavizia vitoto vya 2000's vinavyopenda chipsi.

Wazee mliochelewa kushika pesa tunaomba mtupumzishe huku mjini.
Right Marker
Dar es salaam