Wazee msiokote simu ni hatari, unaweza kujiingiza kwenye matatizo makubwa

Wazee msiokote simu ni hatari, unaweza kujiingiza kwenye matatizo makubwa

Usiokote Simu, wala kununua Simu kwa mtu.
Nenda nunua dukani uchukue na risiti yake.
Maisha bila nidhamu ni adhabu.
 
Nilishaibiwa simu mara mbili na kudondosha ikaokotwa na mtu mwingine nikashindwa kuwakomoa. Simu sikuweka passwords waliendela kuzitumia wala sikufuatilia zaidi ya ku block line tu. Siku hizi nikiona simu imedondoshwa au kusahauliwa siokoti wala kugusa naacha inaokotwa na mtu mwingine. Unaweza kufanya wema kuokota simu ya mtu akiitafute aipate ikawa shida. Hata mimi nikipoteza simu huwa hawanirudishii kwa hofu nitawageuzia kibao badala ya kushukuru. Hata nikiweka dau zuri aliyeikota huizima na kutokomea kusikojulikana
 
Wazee kuna jamaa yetu huku mtaani kaokota simu na amekamatwa juzi. Mwenye simu kasema aliporwa million 250 kwenye begi lililokuwa na simu

Aisee sijui itakuaje hapo wakuu maana polisi wamemshikilia hawautaki hata awekewe dhamana.

Pia soma
- Kwa sasa, kuokota simu si bahati tena bali ni balaa
Mbaya sana. dada mmoja alishuka na begi lenye laptop na simu la kijana aliyemuomba amshikie kwenye daladala. Kijana akaenda kwa wataalamu wanaotress akalipa elfu 60. Begi lilikutwa mbagala ndanindani huko, sebuleni simu inachajiwa. Kaka akasema kulikuwa pia na laki 9 ndani ya begi, ilibidi wachangishane ukoo mzima. Simu ilimponza bidada.
 
Mimi nao Kota hakuna mpumbavu aache simu njiani yan hata iwe kibonteli naibeba
 
Fedha ndiyo kitu pekee unachoweza kukiokota na kusema nayo
Mengine yote ni msalaaa

Ova
 
Wazee kuna jamaa yetu huku mtaani kaokota simu na amekamatwa juzi. Mwenye simu kasema aliporwa million 250 kwenye begi lililokuwa na simu

Aisee sijui itakuaje hapo wakuu maana polisi wamemshikilia hawautaki hata awekewe dhamana.

Pia soma
- Kwa sasa, kuokota simu si bahati tena bali ni balaa
Hizo milioni 250 zina maelezo yoyote? Mzee kafanya biashara gani na kwanini atembee na pesa zote hizo bila escort ya polisi?
 
Back
Top Bottom