William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Buriani sikinde ngoma ya ukae
- mwanzo ilikuwa kama utani pale redio mbao zilipoanza kutangaza kwamba wamiliki wa bendi ya mlimani park orchestra wana sikinde ngoma ya ukae, shirika la mandeleo mkoa wa dar (DDC) wako njia moja kuivunja bendi hiyo kwa kile kilichosemekana kwamba ni mzigo kwa shirika hilo.
- wiki hii imethibitika kwamba habari hizo za kutia uchungu ni za kweli.
hivi tunavyoongea wanamuziki wa sikinde ama nginde nginde hawana ajira, ila inasemekana mwajiri wao amewapa mkono wa dhahabu kwa kuwakabidhi vyombo vya muziki wakajiajiri wenyewe, kama ilivyo msondo ngoma band ambao walijikuta katika jahazi kama hilo baada ya mwajiri wao, jumuiya ya wafanyakazi, kuitema.
- Macho na masikio ya wapenzi wa muziki yanangoja nini kitachofuata, japo wengi wana imani kwamba sikinde haitokufa kutokana na kusheheni nyota wa muziki kama vile hassan rehani bitchuka 'super stereo, na mkongwe shaaban dede.